PIGO SIMBA SC; SALIM KINJE AUMIA, KUWAKOSA PORTS KESHO

PIGO SIMBA SC; SALIM KINJE AUMIA, KUWAKOSA PORTS KESHO

Salim Kinje

KIUNGO Salim Kinje ataikosa mechi ya kesho ya Simba dhidi ya Ports ya Djibouti, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kuwa majeruhi.
Daktari wa Simba SC, Cosmas Kapinga amesema mchana wa jana kwamba, Kinje aliumia misuli kwenye mechi na Azam, Fainali ya Kombe la Urafiki wiki iliyopita na pamoja ya kujilazimisha kuendelea kucheza, lakini imefikia wakati anahitaji mapumziko.
Kapinga alisema leo Kinje ameshindwa kabisa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake na ikabidi afanye mazoezi maalum ya peke yake kulingana na maumivu yake. Kapinga amethibitisha Kinje hatacheza Jumatano na Ports katika mechi ambayo Wekundu wa Msimbazi, wanatakiwa lazima kushinda ili kufufua matumaini ya kuingia Robo Fainali ya michuano hiyo, baada ya kuanza vibaya jana kwa kufungwa 2-0 na URA ya Uganda.

Post a Comment

Previous Post Next Post