Simba, URA sasa Jumapili

BARAZA la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limerudisha nyuma siku moja mechi michuano ya Kombe la Kagame kati ya Simba dhidi ya URA kutoka Jumatatu hadi Jumapili.

Akizungumza na wanahabari Katibu mkuu wa  Cecafa, Nicholaus Musonye alisema mchezo kati ya Simba na URA ya Uganda sasa utafanyika Jumapili.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Jumatatu kutokana na uwanja wa Taifa kutumika kwa fainali ya michuano ya Copa Coca Cola, lakini sasa mechi hizo sasa zimehamishiwa uwanja wa Karume.
Musonye alisema mbali na mechi za Simba na URA pia mechi nyingine itakayochezwa Jumapili ni ile ya Vita Club ya DR Congo dhidi ya Ports ya Djibout ambayo itafanyika  saa nane mchana kwenye uwanja wa Azam Chamazi.

"Katika siku hiyo Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi nyingine itakayoanza saa 10 kamili jioni, itakayowakutanisha wenyeji Azam ya Tanzania Bara dhidi Mafunzo kutoka Zanzibar."

Michuano hiyo itafunguzi wa rasmi hapo kesho saa nane mchana kati ya APR ya Rwanda dhidi El Salam Wau ya Sudan, huku mabingwa watetezi Yanga watashuka dimbani saa 10 jioni kuwakabili Atletico ya Burundi.

Akitangza vingilio katika mchezo huo ni Sh. 5,000 kwa 2,000 kwa mechi ambazo sio za Simba na Yanga wakati zile zitakazohusisha vigogo hao wa Tanzania kingilio cha juu kitakuwa Sh. 20,000.

"Kwa upande wa mechi zinazohusisha Yanga na Simba viingilio vitakuwa kama ifuatavyo; viti vya bluu na kijani sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, viti vya VIP C sh. 10,000, viti vya VIP B sh. 15,000 na viti vya VIP A ni sh. 20,000.

Alisema siku ambazo Simba na Yanga hazichezi, viingilio vitakuwa sh. 2,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya VIP C, sh. 10,000 kwa viti vya VIP B na sh. 15,000 kwa viti vya VIP A. Mashabiki akikata tiketi moja anaona mechi zote mbili; mechi ya saa 8 na ile ya saa 10.

Post a Comment

Previous Post Next Post