TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKABIZI GARI MPYA AINA YA FORD FIGO KWA MSHINDI WAKE.

NI KATIKA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL.
July 3, 2012, Dar Es Salaam: 

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni ijulikanayo kama vumbua hazina chini ya kizibo. Promosheni hiyo inaendeshwa nchi nzima ambapo katika droo ya nne iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni  hiyo zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es Salaam alipatikana mshindi wa gari mpya aina FORD FIGO aliyefahamika kwa jina la Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro.
Leo asubuhi katika ofisi za CMC zilizopo barabara ya azikiwe mkabala na jengo la maktaba square jijini Dar Es Salaam,  mamia ya watanzania kupitia vyombo vya habari wameshuhudia kampuni hiyo ikimkabidhi zawadi hiyo ya gari mshindi wake bwana Isack Juvenary jiji Dar es Salaam.
Akiongea na wandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo amesema “Najisikia faraja kubwa sana ninapoona yale tuliyoyapanga kuyatimiza kwa wateja wetu kama SBL na kwamba hii ni sehemu tu ya yale yoye tuliyopanga kufanya kwa jamii inayotuzunguka kwa kuthamini mchango wa wateje wetu na pia sisi tumelenga katika kuwapa mabadiliko katika maisha yao kwa kuzingatia mahitaji muhimu ya binadamu, na ndiyo maana tuna zawadi za magari, Bajaji, majenerata na pikipiki ili ziwasaidie katika shughuli zao za kila siku na pia fedha taslimu kuanzia shilingi elfu kumi, elfu hamsini na laki moja ambazo unaweza kushinda” alisema Chonjo huku akisisitiza kuwa promosheni hiyo bado inaendelea kwa wiki takriban saba zijazo na kuwataka watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti vya promosheni hiyo kushiriki kwa wingi ili kuongeza uwezo wakushinda zawadi mojawapo.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia chini ya kizibo utapata namba zilizopo katikati ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba hizo mfano 55550, kisha tuma namba zilizopo pembezoni mwa kizibo. Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.  Pia unaweza kujipatia bia ya bure papo hapo kila ubanduapo kizibo cha bia zote tatu zilizoainishwa katika promosheni hii.  Haiuzwi kwa walio chini ya miaka kumi na minane.
Serengeti Breweries Limited ni kampuni tanzu ya EABL/ DIAGEO.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na SBL Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano, Mrs. Teddy Mapunda at teddy.mapunda@diageo.com; Tel +255 784 747 665nakupitiaDrinkQ.com

MWISHO/

Post a Comment

Previous Post Next Post