THOM ASAINI MIAKA MIWILI YANGA, ASEMA HAKUJA KULA BATA, AMEKUJA KUPIGA KAZI
Kocha mpya wa Yanga, Thom Saintfiet jioni hii amesaini
mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu hiyo na baada ya kusaini, akasema
hakuja Tanzania ‘kustarehe’ amekuja kufanya kazi na sera yake ni ushindi. Anataka
ushindi na mataji. Amesema jaribio lake la kwanza ni kutetea ubingwa wa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, katika michuano inayoanza Julai 14, Dare s Salaam
(Habari kamili baadaye). Tazama picha za kusaini kwake Mkataba makao makuu ya
klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
![]() | |
| Kulia ni Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa, katikati Thom anasaini. Kushoto The Don Seif Ahmad 'Magari'Picha na:- http://bongostaz.blogspot.com/ |


Post a Comment