Kocha Villas-Boas anaamini Moutinho, ambaye aliyemfundisha wakati akiwa Porto, ndiye anayeweza kuziba pengo la Modric.
“Alikuwa moja ya wachezaji nyota kwenye michuano ya Euro 2012,” alisema Villas-Boas. “Alikuwa kwenye kiwango kizuri.“Pia, alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Porto katika misimu miwili iliyopita wakati walipotwaa ubingwa wa Ulaya.
“Hiyo ni aina ya wachezaji tunaowataka hapa. Sio kwamba ni mchezaji pekee tunayemfutilia, lakini kama mambo yakienda vizuri tunaweza kumchukua.”
Naye kocha Vitor Pereira amekiri kuwa Moutinho ataondoka Porto msimu huu na kujiunga na Tottenham.
Kocha Pereira alitoa umuhimu wa Moutinho kwenye kikosi chake, na kutishia kwamba atajiuzuru kama kiungo huyo wa Ureno ataondoka na kwenda kujiunga na klabu hiyo ya England.
"Sijazungumza na Villas-Boas, lakini najua kwamba anavutiwa na Moutinho," aliwambia wanahabari. "Na mimi nampenda pia.
"Hapaswi kuuzwa. Nataka endelee kubaki hapa, lakini hii ni soka na kuna uwezakano wa kununuliwa kwa mkataba wote."
Moutinho, ambaye alijiunga na Porto akitokea Sporting Lisbon mwaka 2010 kwa gharama ya euro 11 milioni, na kama Spurs wanataka kumnunu pamoja na mkataka wake wanapaswa kulipwa euro 40 mil kwa mabingwa hao wa Ureno.
Moutinho alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Porto chini ya Villas-Boas, walipotwaa makombe manne msimu wa 2010-11, pamoja na lile la Europa Ligi.
Post a Comment