Vodacom yapunguza gharama za simu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan
· Ni Ofa mpya ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet kwa shilingi 250 tu kwa siku.
· Ofa kuanza kila siku saa tano usiku hadi saa moja asubuhi.
· Kupata ofa hiyo piga *102*250#
Dar es Salaam 25th Julai 2012….
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imeanzisha ofya mpya ya
mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo itawawezesha wateja wa mtandao huo
kupiga simu bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kupata huduma
za intanet kwa shilingi 250/= tu kwa siku.
Ofa
hiyo mpya itakuwa ni kwa siku saba za wiki kuanzia saa tano usiku hadi
saa moja asubuhi katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ili
mteja ajiunge na huduma hiyo, atatakiwa kupiga *102*250# ambapo ataweza
kupiga simu kutoka Vodacom kwenda Vodacom, kutuma ujumbe mfupi wa
maneno kwenda mitandao yote ya simu na kutumia intanet bila kikomo.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania
Bwana Rene Meza alisema kipindi hiki ni maalum kwa waislamu duniani kote
kuwa karibu na Mungu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
“Tumeona
vyema tuwapatie njia rahisi ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki
kwa unafuu na ambayo wataifurahia tukijua kwamba waislamu walio wengi ni
miongoni mwa wateja ambao wametuunga mkono kwa miaka mingi sasa.
Tunataka nao wajisikie kuwa sehemu ya familia ya Vodacom katika kipindi
hiki cha maombi,” alisema Meza.
Ofa
hii imekuja wakati Vodacom Foundation inaendelea na kampeni yake ya
Care and Share mkoani Tanga inayolenga kutoa misaada ya kifedha na vifaa
mbalimbali kwa watoto yatima katika kipindi cha Mwezi wa Ramadhan.
Kampeni
ya Care and Share inaadhimisha miaka mitano tangu kuzinduliwa kwake,
huku ikitoa fursa ya kipekee kwa Vodacom Foundation kushughulikia
changamoto mbalimbali kwa watoto yatima na vituo vya kulelea watoto
yatima.
Kupitia
kampeni hiyo, mamia ya watoto yatima wameweza kusaidiwa na maisha yao
kuboreshwa, suala ambalo jamii nzima na wateja wa Vodacom wanajivunia.
“Tutaendelea
kuwapatia wateja wetu kile wanachostahili kwani bila ya mchango wao
Vodacom Tanzania isingekuwa hapa ilipo leo. Nawatakia waislamu wote
kheri katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan,” alihitimisha Meza.

Post a Comment