WACHEZAJI 11 WAMALIZA MIKATABA COASTAL UNION
Wachezaji
11 wamemaliza mikataba yao ya kuichezea timu ya Coastal Union ya Tanga
inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na sasa wako huru kujiunga na
klabu yoyote.
Kwa
mujibu wa Coastal Union, wachezaji hao ni Ben Mwalala, Samwel Temu,
Francis Busungu, Ahmed Shiboli, Lawrence Mugia, Daudi Chengula, Godfrey
Mmasa, Mwinyi Abdulrahman, Sabri Ramadhan China, Soud Abdallah na
Ramadhan Wasso.
Uhamisho
wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika
Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa
Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
Kwa
klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni
kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia
Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania
imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka
huu) na shirikisho hilo.
Kwa
viwango vya Juni mwaka huu, Tanzania (Taifa Stars) ambayo timu yake
inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 139 hivi sasa
imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni
mwaka huu.
Ivory
Coast inayoshika nafasi ya 16 duniani bado inaongoza kwa upande wa
Afrika ikiwa na pointi 939. Timu hiyo ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo
kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni mabingwa
wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya
kwanza wakiwa na pointi 1,691.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment