WATUMISHI wa Idara ya Elimu mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa na lugha nzuri
ya pindi walimu wanapokwenda kuomba misaada mbalimbali ya kielimu dhidi
ya shule zao pamoja na matitizo yao binafsi kwa ajili ya kuinua kiwango
cha elimu.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoani Ruvuma (CWT), Kastor Ngonyani.
Alisema kuna baadhi ya watumishi wa Idara ya Elimu wamekuwa na lugha ambazo si nzuri.
“Inashangaza kwa baadhi ya maofisa elimu wanawageuka walimu wao kwa kuwanyanyasa bila utaratibu badala ya kuwapa faraja ya utendaji kazi katika shule zao ambazo wamepangiwa na Serikali,” alisema Ngonyani.
Alisema kwa sasa elimu inashuka kiwango kwa sababu ya walimu kutothaminiwa mawazo yao na Serikali pindi wanapotoa ushauri nini kifanyike kuhusiana na suala la elimu.
Naye, mtoa mada katika warsha hiyo, Mwalimu Samwa Mhaiki, alisema changamoto nyingi inayowakabili wataalamu wa elimu ni baadhi ya shule kuanzishwa kisiasa bila kujali taratibu na kanuni, jambo ambalo huchangia ushukaji wa kiwango cha elimu.
Kwa upande wake, Mratibu wa Elimu Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, Dunstan Mshanga, alisema shule nyingi zimesahaulika kwa kutotembelewa na wakaguzi kwa ajili ya kubaini matatizo.
Naye, Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupigania Haki za Mtoto wa Kike Mkoa wa Ruvuma, Anna Tembo, alisema inatakiwa Serikali iangalie upya namna ya kumtumia mtoto wa kike katika sherehe mbalimbali, hasa wakati wa kucheza ngoma za unenguaji mbele ya halaiki kwa lengo la kunogesha sherehe.
“Tunakutana na changamoto kubwa dhidi ya watoto wa kike kwa kuwekwa mimba za utotoni ambazo hazikutarajiwa na kufanya mtoto huyo kushindawa kumudu masomo yake,” alisema Tembo.
Alisema shule nyingi hazina vyumba vya faragha kwa ajili ya kuelimishia watoto hao pindi wanakupokuwa wanahitaji msaada kulingana na maumbile yao.

Source;- Mtanzania
Post a Comment