RASMI IBRA ATUA PSG
![]() |
Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa, imetangaza rasmi
kukamilisha usajili wa Zlatan Ibrahimovic (pichani) kutoka AC Milan ya Italia. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Sweden, amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamuweka
Parc des Princes hadi mwaka 2015, huku klabu hiyo ya Mji Mkuu wa Ufaransa,
ikiripotiwa kutumia kiasi cha Euro Milioni 23 kuinasa saini ya mpachika mabao
huyo wa zamani wa Inter Milan ya Italia pia na Barcelona ya Hispania.
|

Post a Comment