AFC LEOPARDS YA KENYA KUKIPIGA NA SIMBA, YANGA IDD EL FITR
TIMU
ya soka ya AFC Leopards ya Kenya inatarajiwa kuja nchini wiki hii
kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Simba na Yanga.
Mechi
hizo mbili zimeandaliwa na Kampuni ya Dar Solutions kwa ajili ya kuzipa
mazoezi Simba na Yanga zinazojiandaa kwa michuano ya ligi kuu ya
Tanzania Bara.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Kenny
Mwaisabula alisema mjini Dar es Salaam leo kuwa, AFC Leopards itacheza
mechi yake ya kwanza Agosti 19 kwa kupambana na Simba kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Kwa mujibu wa Mwaisabula,
AFC Leopards itajitupa tena uwanjani Iddi Pili (Agosti 21) kwa kumenyana
na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Mwaisabula alisema timu ya Coastal Union inatarajiwa kupimana ubavu na Chemili ya Kenya katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa siku ya Iddi Mosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
Post a Comment