ARSENAL WAKUBALI YAISHE. SASA WATAKA BILIONI 55 WAMUACHIE VAN PERSIE KWA MAN U
LONDON, England
HATIMAYE klabu ya
Arsenal iko mbioni kumuuza nahodha wao Robin van Persie kwa mahasimu
wao Manchester United kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England Jumamosi.
Gazeti la The Sun limesema leo kuwa Arsenal walikuwa wanajiandaa kutangaza uamuzi utakaoashiria kuwa wamekubali yaishe na kufikia muafaka katika 'dili' la kumuuza Van Persie kwa Man U.
Sasa Arsenal wanajiandaa kufanya mazungumzo ya kina na kocha Alex Ferguson wa Man U, wakitarajia kumuachia kwa paundi za England milioni 22 (Sh. bilioni 55) kabla ya ufunguzi wa mechi za za msimu mpya wa Ligi Kuu ya England Jumamosi.
Hata hivyo, Man U na mabingwa wa Italia, Juventus bado hawajaongeza dau walilotangaza awali la paundi za England milioni 15 (Sh. bilioni 37).
Hata hivyo, Van Persie (29), alizomewa na mashabiki wa Arsenal Jumapili wakati waliposhinda mechi yao ya kirafiki dhidi ya Cologne nchini Germany na sasa ana usongo wa kutaka kuondoka. Zaidia soma:- straikamkali
Robin Van Persie |

Post a Comment