AZAM WATAKA MILIONI 50 KWA REDONDO
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba SC; Zakaria Hanspop |
MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC, hivi sasa wanakwenda
mbio kwa kasi ya Usain Bolt kukamilisha usajili wao, kabla ya dirisha kufungwa
kesho.
Azam FC wanataka Sh. Milioni 50 kabla ya dirisha la usajili
kufungwa saa 6:00. usiku kesho ili kumuachia kiungo Ramadhan Chombo ‘Redondo’
kesho na hivi sasa Simba SC wapo kwenye kikao kizito kujadili namna ya
kukamilisha usajili wao, kabla ya dirisha hilo kufungwa.
Mapema leo, asubuhi http://bongostaz.blogspot.com/ iliripoti kwamba, Azam
imekubali kupokea Sh. Milioni 15 kutoka Simba SC ili kumuuza Redondo wa Ngomati
kwa Wekundu hao wa Msimbazi, lakini baada ya kuzama ndani, upande wa pili,
imegundua zinatakiwa Milioni 50 za Tanzania. Zaidi bofya hapa
Post a Comment