CAMP NOU YAMNYAKUA SONG, SAHIN AJA EMIRATES KUZIBA PENGO LAKE.
Alex Song anaenda Barcelona |
KIUNGO
wa kimataifa wa Cameroon, Alex Song anatarajiwa kutua Barcelona leo
kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 15 katika klabu hiyo ya Nou Camp -
wakati huo huo, Arsenal inakwenda mbio kukamilisha usajili wa mkopo wa
Nuri Sahin kutoka Real Madrid, awe mbadala wake.
Arsenal
inajiamini itampata Sahin wiki ijayo kutokana na kiungo wa Uturuki,
ambaye pia ana pasipoti ya Ujerumani kuonyesha nia ya kujiunga na klabu
hiyo ya London, kuliko Liverpool, ambao pia wanamtaka.
Real
Madrid pia kwao ni bora Sahin aende Anfield kwa sababu watapata ada
kubwa ya mkopo, lakini watapingana na nia ya mchezaji kutaka kwenda
Emirates.
Arsenal
pia inatumai, winga Theo Walcott atasaini mkataba mpya mwezi ujao,
kutokana a mkataba wake wa sasa kuwa inausha mwishoni mwa msimu na
mazungumzo yanaendelea.
Klabu
hiyo inafikiri wachezaji wapya Lukas Podolski, Santi Cazorla na Olivier
Giroud, watamshawishi kubaki, licha ya Robin van Persie
kuondoka. Arsenal inaweza kusajili kiungo mwingine mkabaji, kutoka
Rennes, Yann M'Vila kwa dau la pauni Milioni 8.
Kocha
Arsene Wenger alisema: "Tutasajili kiungo mwingine. Lazima tuwe
vizuri.' Song, mwenye umri wa miaka 24, aliyejiunga na Arsenal akiwa
ana umri wa miaka 18 kutoka Bastia , mwaka 2005, atakamilisha uhamisho
wake leo na Barca inatumai kumtangaza rasmi kesho.
Akifafanua
juu ya uamuzi wa kumuacha Song aondoke, Wenger alisema: 'Ameonyesha nia
yake ya kwenda Barcelona. LakiniJack Wilshere anarudi ndani ya mwezi
mmoja na nusu. Pia tuna Abou Diaby, ambaye amerejea baada ya kupona
maumivu yake, na Tomas Rosicky hayuko mbali.
'Inachanganya
(wachezaji wanapoondoka) lakini tumejifunza kupambana na hali hiyo, na
ushawishi wa kifedha wa klabu nyingine ni mkubwa. Mbalo linafanya
tofauti.'
Song
anatakiwa na Barca akawe msaidizi wa Sergio Busquets na walipandisha
dau lao baada ya mchezaji ambaye walimtaka awali kama chaguo lao la
kwanza, Javi Martinez, anataka kwenda Bayern Munich kwa pauni Milioni 35
Nuri Sahin wa Real Madrid atatua Arsenal kwa mkopo
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
Post a Comment