COASTAL YAPIGWA 2 - 0 MKWAKWANI NA BANDARI, MGUNDA, KONDO WAKALIA KUTI KAVU

COASTAL YAPIGWA 2 - 0 MKWAKWANI NA BANDARI, MGUNDA, KONDO WAKALIA KUTI KAVU

 Makocha wa Coastal, Juma Mgunda kulia na Msaidizi wake, Habib Kondo kushoto

COASTAL Union imefungwa mabao 2 - 0 jana jioni hii na Bandari ya Mombassa, Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Mabao ya Bandari inayocheza Ligi Daraja la Kwanza Kenya, yalitiwa kimiani na kiungo David Naftali dakika ya 27 kwa shuti la umbali la mita 35, baada ya kupewa pasi na mshambuliaji Thomas Marucie, wote Watanzania.
Bao la pili lilifungwa na Evan Wandela dakika ya 88 kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na Hussein Puzzo.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Coastal waliwatia kashikashi makocha Juma Mgunda na Msaidizi wake Habib Kondo wakidai hawafai na kutaka waondolewe, hali ambayo ilifanya waondolewe uwanjani kwa msaada wa Polisi.
Hali hii inajitokeza kwa mara ya pili, baada ya juzi pia timu hiyo ikicheza na JKT Oljoro ya Arusha pamoja na kushinda bao 1-0, mashabiki walilalamikia kiwango kibovu na kuzomea makocha. Jumamosi, Coastal itacheza Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post