HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOWAPIKU SIMBA KATIKA USAJILI WA AKINA TWITE
PACHA; Mbuyu (kushoto) na Kabange (kulia) wanakuja Yanga |
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imeifanyia kitu mbaya sana
Simba SC ambacho hawataamini maisha yao yote.
Kitu gani hicho? Ni kumsajili Mbuyu Twite na kumrudisha
kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya
Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini humo na kumbadili jina pia.
Kwa kumbadili uraia, Yanga wamepata na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), wakati huo huo, Simba
wanahangaika kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la
Rwanda.
Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo,
klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake,
Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba, APR ilimuuza Mbuyu tena
kurejea Lupopo, ambao sasa wanamuuza Yanga.
Habari za kiuchunguzi, ambazo chanzo imezipata
zinasema kwamba, Simba ilimsaini beki huyo wa APR kupitia Mwenyekiti wake,
Alhaj Ismail Aden Rage, kwa dola za Kimarekani, 10,000, lakini Yanga baadaye
wakampandia dau.
Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake Mbutu
(pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao
kucheza timu moja daima.
Huko nyuma, Yanga iliwahi kuifanyia tena Simba ‘umafia’ kama
huu katika usajili wa wachezaji, Charles Boniface Mkwasa na Yussuf Ismail Bana,
miaka ya 1980.
Simba ilimsaiji beki wa Pamba kama Yussuf Bana, lakini Yanga
wakaingilia kati na kumsajili kwa jina la Yussuf Ismail Bana, Mwenyekiti wa
Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa Shirikisho, TFF), wakati huo Said Hamad El
Maamry akamuidhinisha beki huyo kucheza Yanga.
Simba walijaribu kumuiba kiungo Charles Boniface, aliyesajiliwa
Yanga kutoka Tumbaku ya Morogoro na kumsajili, lakini baadaye Yanga wakamsajili
pia na kumbadili jina, wakimpa Charles Boniface Mkwasa.
Mkwasa alifungiwa na FAT ya El Maamry kabla ya kufunguliwa
baadaye na kuendelea kukipiga Yanga.
Chanzo:- http://bongostaz.blogspot.com/
Post a Comment