Jerry Silaa achukua fomu kuwania nafasi ya uongozi UVCCM-NEC
Naibu
katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally (kulia) akimkabithi
fomu za kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa jana katika ofisi za CCM mkoa mjini
Magharibi Zanzibar, katikati ni Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa
Kusini unguja akishuhudia tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi
zinazogomewa kua ni Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu, Wajumbe wa
Baraza Kuu na wajumbe wa Halmashauri. Hata hivo mstahiki meya wa
manispaa ya ilala alipohojiwa hakuweka wazi nafasi gani anayotaka
kugombea kwani alikua bado anakusanya maoni na ushauri kutoka watanzania
mbalimbali na kujipima mwenyewe ni nafasi ipi itakayo mfaa zaidi ili
kuweza kuwatumikia wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa karibu
zinasema mstahiki meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM-NEC.
Post a Comment