KIJANA APOTEZA MAISHA PAPO HAPO MARA BAADA YA KUKANYAGWA NA LORI NA KUPELEKEA KICHWA KUPASUKA NA UBONGO KUTOKA

Baadhi
ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza
maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na
hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo majira
ya saa tisa mchana eneo la ilala boma


Mwili
wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa
umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni
mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea kichwa
kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana
eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa
la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.

Askari
wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili
wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili
kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana
huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi
Msimbazi.

Baadhi
ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na
kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.

Mwili
wa marehemu ukifunikwa vizuri kwaajili ya kupelekwa hospitali ya
amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni vipande vya ubongo mara baada ya
kukanyangwa na lori
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Kijana
wa kiume ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amepoteza
maisha mara baada ya kugongwa na lori leo majira ya Saa tisa Mchana eneo
la Ilala Boma karibia na Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa Dar Es salaam. Mara
baada ya kugongwa na lori, lori hilo liliweza kukimbia na halikujulikana
ni wapi limeelekea na namba za gari hizo hazikuweza kupatikana mara
moja.
Kijana
huyu anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 ambaye pia shuhuda wa ajali
hii ameueleza mtandao wa lukaza blog kuwa ni mwanafunzi wa shule ya
msingi Msimbazi Center kutokana na sare za shule alizokuwa amevaa.
Shuhuda
wa Ajali hii ambaye hakupenda jina lake kuchorwa na mtandao wa LUKAZA
amesema kuwa Wakati kijana huyo anavuka barabara lori lililomgonga
lilikuwa linatokea maeneo ya buguruni na kumgonga kijana huyo. Mara
baada ya kumgonga lilimkanyaga kichwani " Lilianza tairi la mbele
kumkanyaga kichwa halafu likafuatia na tairi la nyuma ambapo lilipelekea
kichwa kupasuka vibaya na hatimaye ubongo kusambaa barabarani kama
ambavyo unao hapo chini na hatimaye lori hilo kukimbia" alisema shuhuda
huyo.
LUKAZA BLOG ilimuuliza shuhuda huyo kwanini akunakili namba za usajili wa lori hilo
na
hivi ndivyo shuhuda wetu alivyojibu " Kiukweli Nilishindwa kuandika au
kunakili namba ya usajili wa lori kwasababu kwanza niliposikia kitu
kizito kimegongwa na hilo lori nilijua ni mtu wa bodaboda wakati
naangalia vizuri nikaona ni kijana mdogo ndiye amegongwa na lori
likimkanyaga kichwa likiwa katika harakati ya kukimbia hapo nilishindwa
kuandika chochote kwasababu nilipigwa na butwaa na kubaki kama bumbuwazi
na mwili kushikwa na ganzi mara baada ya kuona ubongo vipande vya
ubongo chini" alisema shuhuda wetu
Mpaka
mtandao wa lukaza blog unaondoka eneo la tukio lori lililomgonga
halikuweza kupatikana wala kujulikana lilipoelekea na jina la kijana
aliyepoteza uhai papo hapo nalo halikuweza kupatikana
Lukaza blog
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZO JUU
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEPA PEPONI AMINA
Post a Comment