LIVERPOOL YAPIGA 3-1, ANDY CARROLL AKIFUNGA BAO LA KUMTAHADHARISHA BRENDAN RODGERS
MSHAMBULIAJI
Andy Carroll amemkumbusha uwezo wake kocha Brendan Rodgers anayetaka
kumuuza, baada ya kufanya mavituz katika mechi ya mwisho ya Liverpool ya
kujiandaa na msimu mpya.
Mshambuliaji
huyo wa England, ambaye mustakabli wake umekuwa haueleweki katika
dirisha hili la usajili, aliingia akitokea benchi kipindi cha pili na
kutoa mchango mzuri akifunga bao kwa shuti la mita 20 dakika ya 66 na
kuifanya Liverpool iongoze 3-0.
Ingawa
Sidney Sam alipunguza bao moja kwa Bayer Leverkusen, Liverpool haikuwa
kwenye hatari yoyote katika siku ambayo Raheem Sterling alicheza na
kufunga bao la kwanza kabla ya Lucas Leiva kufunga na pili.
Andy Carroll anafunga
Nyumbani tena: Sami Hyypia amerejea Anfield kama kocha wa Bayer Leverkusen
Lucas Leiva akishangilia
Raheem Sterling akishangilia baada ya kufunga la kwanza
Carroll akipaa hewani kupiga kichwa kilichoota mbawa
SOORCE: http://www.dailymail.co.uk
Post a Comment