ROONEY AUZWA PAUNI MILIONI 40
Wayne Rooney anahofia Manchester United inajiandaa kumuuza kwa
pauni Milioni 40. Na hofu hiyo inakuja baada ya kusajiliwa Robin van
Persie kutoka Arsenal.
Habari kamili: Daily Mirror
Winga wa England, Theo Walcott amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya
Arsenal na anaweza kuuzwa kwa pauni Milioni 15 na klabu za Manchester
City na Liverpool zipo mstari wa mbele kumsaini nyota huyo mwenye umri
wa miaka 23.
Newcastle itakubali ofa za kuwauza beki Muargentina, Fabricio
Coloccini, mwenye umri wa miaka 30, kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast,
Cheick Tiote, mwenye umri wa miaka 26, au kiungo Mfaransa, Yohan Cabaye,
mwenye miaka 26 pia.
Habari kamili: Independent
Wakala wa Dimitar Berbatov amekwenda Florence kufanya mpango wa
uhamisho wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Bulgarian kutoka
Manchester United kwenda Fiorentina.
Habari kamili: Gazetta dello Sport (in Italian)
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amemuonya Stewart Downing
kwamba winga huyo anaweza kurudishwa beki ya kushoto ili kupata nafasi
ya kuendelea kuishi Anfield.
Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta ameelezea jinsi alivyochanganyikiwa na
jinsi wachezaji wapya wanavyokabiliwa na changamoto ya kuchanganya
haraka, baada ya kuondoka kwa nyota Robin van Persie.
Habari kamili: Metro
Post a Comment