Magufuli Atangaza ‘Maumivu’ Barabara Ya Morogoro
WAKAZI
wa Jiji la Dar es Salaam hususan maeneo ya karibu ya Barabara ya
kwenda Morogoro wametakiwa kukaa chonjo kutokana bomoabomoa
itakayozikumba nyumba mbalimbali ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo
kwa urefu wa kilometa 200 kutoka jijini kwenda Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema hayo jana alipozungumza kwenye
mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Kitivo cha Uhandisi
na Teknolojia jijini hapa.
Alisema barabara hiyo inatarajiwa kujengwa njia sita umbali wa kilometa 200 kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.
Waziri
aliwatahadharisha watu waliojenga kwenye hifadhi ya barabara waanze
kuondoka ili kupisha upanuzi huo kabla hawajaondolewa kwa nguvu.
“Wote waliojenga kwenye hifadhi ya barabara waanze kujiandaa kuondoka kwasababu sheria ni msumeno,”alisema Dk Magufuli.
Akizungumzia
wahitimu walitunukiwa shahada na stashahada jana hiyo, aliwataka
wahitimu hao kwenda kufanya kazi kwa kusimamia sheria na kuzikabili
changamoto zilizopo katika jamii.
“Mkubali
changamoto hata kama ni kwa kulaaniwa maana ni afadhali kuuawa kwa
kukataa rushwa kwasababu utakuwa umelikomboa taifa,”alisema.
Pia
alimwagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi, Profesa Ninatubu Lema
kuwapatia usajili wanafunzi wote waliohitimu chuoni hapo na wale
wanaoendelea na masomo ili watakapokuwa wanatafuta kazi wasisumbuliwe.
Alisema
hadi sasa kuna wahandisi 11,400 waliosajiliwa na makandarasi 9,126.
Pia waziri huyo alitoa zawadi ya Sh1 milioni kwa wahitimu waliofanya
vizuri katika masomo yao.
Post a Comment