MCHAKATO WA SERENGETI FIESTA 2012 WAENDELEA KUPAMBA MOTO NDANI YA JIJI LA TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Dr Msengia  akiaga baada ya kuitembelea timu Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Kilimanjaro jioni ya leo. Katikati ni Erick Kussaga ambae ni Mzalishaji wa timu ya Fiesta mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Mheshimiwa Dr Msengi akiwa na Afisa Uhusiano wa Clouds Entertainment Co. LTD kwa upande wa Viongozi wa Taasisi za Serikali na Vyama vya Siasa Ndugu Simalenga Simon wakati Mkuu huyo wa Wilaya alipoitembelea timu ya amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Mkoani Kilimanjaro jioni hii.Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linatarajia kuzinduliwa rasmi kesho katika uwanja wa chuo cha Ushiriki mkoani humo,ambapo msanii nyota kutoka nchini Kenya,CMB Prezoo ataliongoza jahazi la wasanii mbalimbali kutoka hapa nyumbani,katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 5000 kwa kila kichwa. 
Mmoja wa washabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta damu akiwa na fulana yake ya tamasha hilo lililowahi kufanyika mjini moshi lililopachikwa jina la jipanguze kama uonavyo pichani.Wanaharakati anuai wa tamasha la serengeti fiesta 2012 leo wameamsha amsha wakazi wa mji huo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Himo,Stendi kuu ya mabasi pamoja na soko la Mbuyuni na kutoa zawadi ya mafuta ya gari/pikipiki na bajaji kutoka kampuni ya Gapco ambayo ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo,kwa watu kadhaa ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za awali ya tamasha lenyewe.
 Mchakato wa Serengeti Fiesta 2012 ndani ya Tanga ukiendelea ndani ya mitaa kadhaa ya jiji hili. Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, hapa vijana wa kazi kutoka Clouds Fm wakiongea na wakazi wa eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 26.8.2012 katika uwanja wa Mkwakwani.
 Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, akiyaendeleza mastori ndani ya kitaa cha Taili tatu eneo la Magaoni, Kata ya Mabawa, Tanga.
 Mwanadada Loveness Love akiwa na Gossip Cop Tz, Sudi Brown.
 ...Wakionyesha umahili wao wa kunwaga.
 ... aha... mimi ni msela siwezi kwenda jela...
 ... vijana walijitahidi kuonyesha umahili wao wa kuchana michano.
 ... Clouds Tv nayo haikukosa.
 Rasi akionyesha umahili wake wa  kuimba rege.
 Adamu Mchomvu akisababisha mambo.
 Gossip- Cop Tz Sudi Brown akiwa katika pozi.
 Mazungumzo ya mtaani yakiendelea.
 Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu na Mwanadada Loveness Love.
 ...hata jamaa alikuwa akitiririka machache ndani ya Clouds Fm/Clouds TV.
 Producer wa Home record ya Tanga nae akimwaga madini.
 Show Love ikiendelea.
 Show love ndani ya eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa.
Aha! Mzee wa Habari na Matukio (Kajunason Blog) akiwa na Adamu Mchomvu wakiwakilisha na chama la watoto wa Tanga

Post a Comment

Previous Post Next Post