MILOVAN ATUA, VIFAA VIPYA MSIMBAZI VYAANZA MAZOEZI

MILOVAN ATUA, VIFAA VIPYA MSIMBAZI VYAANZA MAZOEZI


Simba mazoezini Coco. Picha na Saleh Ally
KOCHA wa Simba SC, Mserbia Milovan Cirkovick amerejea usiku wa kuamkia leo kutoka kwao Serbia, alipokuwa kwa mapumziko mafupi, baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambayo timu yake ilitolewa katika hatua ya Robo Fainali kwa kufungwa 3-1 na Azam FC.
Habari/picha na:- Saleh Ally
Milovan anatarajiwa kuendelea sasa na kazi ya kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayoanza mwishoni mwa mwezi huu, akianza na mechi ya Ngao ya Jamii, dhidi ya Azam FC.
Wakati Milovan akitua jana, mahudhurio ya mazoezi ya Simba ambayo pia itashiriki Kombe la Banc ABC Super 8, michuano inayoanza kesho, bado si mazuri.
Ni wachezaji 16 tu waliohudhuria mazoezi ya asubuhi ya leo, ufukwe wa Cocoa Beach, Oysterbay, Dar es Salaam, wakiwemo wawili wapya, Mrisho Khalfan Ngassa kutoka Azam FC na Cassian Ponella kutoka Kagera Sugar.
Waliofanya mazaoezi leo ni Juma Kaseja, Hamadi Waziri, Shomary Kapombe, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paul Ngalema, Juma Nyosso, Cassian Ponella, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Kanu Mbivayanga, Mrisho Ngassa, Haruna Moshi, Haruna Shamte, Kiggi Makassy na Salim Kinje.

Post a Comment

Previous Post Next Post