OCHIENG, KINJE HATIHATI KUCHEZA SIMBA, ITC ZAO BADO MGOGORO
![]() |
Paschal Ochieng kulia akikabidhiwa jezi ya Simba na Zacharia Hans Poppe, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'. |
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
kwa wachezaji 11 wa nje kati ya 14 walioombea usajili na klabu
mbalimbali za Ligi Kuu, huku Salim Kinje na Paschal Ochieng wa Simba
wakiwa bado ITC zao hazijapatikana.
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura amesema
kwamba wachezaji walioombewa usajili Yanga na tayari ITC zao
zimepatikana ni Nizar Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada,
Didier Kavumbagu (Atletico Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC
Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wambura
alisema kwa upande wa Simba ni Musa Mude (Sofapaka, Kenya) na Daniel
Akuffor (Stella Abidjan, Ivory Coast) wakati Mtibwa Sugar ni Shaaban
Kisiga timu ya El Itihad ya Oman.
Alisema waliopata
ITC kwa upande wa Kagera Sugar ni Wilfred Ojodale Ame na Benjamin Efe
Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya Nigeria. Wengine ni Deangelis Silva
kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal Union, George Odhiambo kutoka
Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na Jerry Santo kutoka Tusker,
Kenya kwenda Coastal Union.
Alisema
wachezaji ambao wameombewa usajili na ITC zao bado hazijapatikana ni
Salum Kinje na Pascal Ochieng wa AFC Leopards, Kenya kwenda Simba na
Ayoub Hassan Isiko kutoka Bull FC, Uganda kwenda Mtibwa Sugar.
Bado
klabu ambazo hazijakamilisha usajili na kupata ITC zina fursa ya
kufanya hivyo hadi Septemba 4 mwaka huu ambapo dirisha litafungwa.
Pia
TFF imetoa ITC kwa wachezaji wanane walioombewa kwenda kucheza mpira wa
miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji kutoka katika klabu mbalimbali
za hapa nchini.
Wachezaji
hao na klabu wanazokwenda katika mabano ni Abdallah Ally Abdallah (CD
Madchegde, Msumbiji), Almasi Khatib Mkinda (Ferroviario da Beira,
Msumbiji), David Naftali (Bandari, Kenya) na Hassan Hassan Mustafa (CD
Madchegde, Msumbiji).
Wengine
ni Meshack Abel (Bandari, Mombasa), Mohamed Banka (Bandari, Kenya),
Thobias Davis Silas (CD Madchegde, Msumbiji) na Thomas Maurice (Bandari,
Kenya).
Wakati
huo huo: Klabu zote zilizowasilisha TFF maombi ya usajili kwa wachezaji
wao zinatakiwa pia kuwasilisha nakala za hati zao za vipimo vya afya
(medical certificate) kwa mujibu wa kanuni za usajili.
Post a Comment