SAMATTA ATUPIA, MAZEMBE YAICHAPA 2-0 ZAMALEKE

SAMATTA ATUPIA, MAZEMBE YAICHAPA 2-0 ZAMALEKE


Samata Goal
MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jioni hii wamefufua matumaini ya ubigwa wa tano wa michuano hiyo, baada ya kuifunga Zamalek ya Misiri mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa TPM, mjini Lubumbashi.
Shukrani kwao, N. Kasongo aliyefunga bao la kwanza dakika ya 70, akimalizia pasi ya D. Kanda na Mbwana Ally Samata aliyeongeza la pili dakika ya 77, akiunganisha pasi Tressor Mabi Mputu. Habari na http://bongostaz.blogspot.com/
Mazembe sasa imefikisha pointi nne, baada ya awali kufungwa na Al Ahly ya Misri mjini Cairo 2-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Berekum Chelsea ya Ghana nyumbani, Lubumbashi.
Mechi nyingine ya kundi hilo leo kati ya Ahly inayoongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, na Chelsea ya pili yenye pointi nne, mjini Cairo itachezwa baadaye saa 5:00 usiku. Zamalek haina pointi na inashika mkia.

MSIMAMO WA KUNDI B LA AKINA SAMATTA AFRIKA:
KUNDI B
                                   P   W       D        L        GF      GA     GD     Pts
1   Al Ahly                   2   2         0         0         3        1         2         6
2   Berekum Chelsea    2   1         1         0         5        4         1         4
3   TP Mazembe           3   1         1         1         5        4         1         4
4   Zamalek                  3   0         0         3         2        6         -4       0

MECHI NYINGINE LEO AFRIKA:
Al Ahly   v   Berekum Chelsea         (Saa 5:00 usiku, Cairo)

Post a Comment

Previous Post Next Post