SHEIKH NURDIN KISHKI ALAANI TABIA YA KUSHEREHEKEA IDDI KWA DISKO, NGOMA, MUZIKI WA DANSI, ULEVI, ZINAA... !
|
Sheikh
Nurdin Kishki akitoa mawaidha kwa waumini wa Kiislamu baada ya
kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga
jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Baadhi
ya waumini wa Kiislamu wakisikiliza mawaidha kutoka kwa Sheikh Nurdin
Kishki kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam,
leo. |
|
Sehemu
ya mamia ya waumini wa Kiislamu wakifuatilia mawaida kutoka kwa Sheikh
Nurdin Kishki kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es
Salaam, leo. |
|
Baadhi
ya akina mama wakisikiliza mawaidha na wengine wakiondoka baada ya
kuswali Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es
Salaam, leo. |
|
Baadhi
ya akina mama wakisikiliza mawaida kutoka kwa Sheikh Nurdin Kishki
baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe
-Yanga jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Haa
haa haaaa....leo ni ubwabwa tu! Mtoto Muzzammil akionekana mwenye
furaha tele baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya
Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Halo halooo....! Watoto hawa pia walikuwa wenye furaha baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Watoto
Luqman (kulia) na mdogo wake Muzzammil wakijiandaa kurejea kwao baada
ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga
jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Leo
pilau tu...! Mtoto huyu anaonekana kama anayetafakari baada ya
kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga
jijini Dar es Salaam, leo. |
|
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. |
|
Waumini akina mama wakiwa kwenye swala ya Idi visiwani Zanzibar leo. |
|
Makamu
wa Rais, Dk. Ghalib Mohamed Bilal akizungumza na waumini baada ya swala
ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. |
|
Rais
Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kulia) akisalimiana na waumini baada ya
kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam leo. |
|
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (wa nne
kushoto) akiswali Idi visiwani Zanzibar leo. Wa pili kushoto ni Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Pandu Ameir Kificho. |
|
Mufti
wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Said Mwambungu wakati wa swala ya Idi iliyofanyika kitaifa
mkoani Ruvuma leo. |
|
Bango
linaloashiria onyesho katika siku ya Idi leo katika ukumbi mmoja uliopo
Tandika Maguruwe jijini Dar es Salaam leo... kusherehekea Idi kwa
mtindo huu ndiko kulikokatazwa na Sheikh Kishki leo. |
|
Tangazo
hili nalo nd'o yaleyale yanayolaaniwa na Sheikh Kishki kwani mwishowe
huambatana na matendo ya kumkufuru Mwenyezi Mungu... hapa ni katika
ukumbi mmoja uliopo Tandika Maguruwe jijini Dar es Salaam.
|
Mhadhiri maarufu wa dini ya Kiislamu
nchini, Sheikh Nurdin Kishki, amelaani tabia ya kusherehekea sikukuu ya
Idi kwa matamasha hafla na matamasha 'kharamu' ya ngoma, disco, muziki
wa dansi, taarabu, bongofleva, ulevi, zinaa na matendo mengine
yanayokwenda kinyume na mafundisho ya dini hiyo.
Akizungumza na
mamia ya waumini walioshiriki ibada ya swal ya Idi kwenye viwanja vya
Tandika Mwembe-Yanga leo asubuhi, Sheikh Kishki alisema kuwa
kusherehekea sikukuu ya Idi kwa vitendo vya aina hiyo ni makosa makubwa
na kwamba humchukiza Allah, Muumba wa Mbingu na Ardhi.
"Wamelaaniwa wale wote wanaosherehekea sikukuu hii kwa matendo maovu," alisema Sheikh Kishki.
"Hawa
wanaofanya vitendo vya kumuudhi Mwneyezi Mungu katika siku kama ya leo
wajiandae kwa adhabu kali siku ya kiama... tuwaombee dua ili waache na
wale watakaoendelea basi wajiandae kupata laana za Mwenyezi Mungu,"
alisema Sheikh Kishki.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ghalib Mohamed Bilal, amewaombaa
waumini wa dini ya Kiislamu kushiriki katika zoezi la sensa kwani ni
muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Dk. Bilal aliyasema hayo baada ya swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Hivi
karibuni, wanaharakati kadhaa wa Kiislamu, akiwemo Sheikh Ponda Issa
Ponda, wamekaririwa mara kadhaa wakisema kuwa Waislamu hawatashiriki
sensa ikiwa katika madodoso hakutakuwa na kipengele cha dini. Ponda na
wanaharakati wenzake waliamua kutangaza msimamo huo baada ya hivi
karibuni, Televisheni ya Taifa (TBC1) kuutangazia umma wakati wa sherehe
za miaka 50 ya uhuru kuwa nchi hii ina Wakristo asilimia 52, Waislamu
asilimia 32 na watu wa dini nyingine asilimia 14; takwimu ambazo
zilibainika kuwa ni za kupikwa kwani hakuna sensa yoyote iliyowahi
kufanywa nchini na kuonyesha matokeo ya aina hiyo.
Ili kukomesha
vitendo vya aina hiyo, ndipo Sheikh Ponda na wanaharakati wengine ambao
wanaamini Waislamu ndio wengi zaidi walipoitaka Serikali iweke kipengele
cha dini katika madodoso ya sensa ili kujua ukweli ni watu wa dini gani
walio na idadi kubwa zaidi nchini.
Hata hivyo, TBC kupitia
mkurugenzi wake Clement Mshana ilishaomba radhi kutokana na upotoshwaji
uliofanywa na kituo hicho, ikisema kwamba mhusika aliyetoa taarifa hizo
potofu ameshachukuliwa hatua ya kuonywa.
Swala ya Idi kitaifa leo iliswaliwa mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mufti Shaaban Issa Simba.
Post a Comment