TAIFA STARS YAUA TAIFA CUP
![]() |
Taifa Stars |
MICHUANO
ya Kombe la Taifa (Taifa Cup) inayoshirikisha kombaini za mikoa ya
Tanzania Bara haitakuwepo mwaka huu kutokana na kukosekana kwa udhamini.
Taarifa
ya TFF imesema licha ya kukosekana kwa udhamini, awali walifikiria
kuendesha mashindano hayo kwa michango ya wanachama wetu (vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa) na Serikali za mikoa kugharamia timu zao.
Lakini
baadhi ya wanachama wetu na Serikali za mikoa walishauri kuwa ni ngumu
kuendesha mashindano hayo kwa sasa kutokana na shughuli za kitaifa
zinazoendelea hivi sasa ikiwemo maandalizi ya sensa ya watu na makazi.
Kwa
mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
mashindano ya Kombe la Taifa yalitakiwa kufanyika kuanzia Julai 23 hadi
Agosti 6 mwaka huu.
Michuano
ya Kombe la Taifa msimu uliopita ilidhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao sasa ni
wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars na Mbeya waliibuka mabingwa
katika fainali iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri
Abeid jijini Arusha.
Wakati TBL wanadhamini Taifa Cup, kampuni nyingine ya bia nchini, Serengeti (SBL) ndio walikuwa wadhamini wa Taifa Stars.
Post a Comment