CRISTIANO Ronaldo amemweleza rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwamba anataka KUONDOKA, imebainishwa.
Radio Cadena COPE imesema Ronaldo alikutana na Florentino Jumamoso usiku na kumfahamisha kwamba hana furaha na anataka kuuzwa.

Jana, licha ya kufunga mara mbili katika ushindi wa 3-0 didi ya Granada, Ronaldo alichafua sherehe kwa kutangaza kwamba "hakuwa na furaha" na kwamba jambo hilo linatokana na matatizo katika weledi wa kazi yake - na si maisha yake binafsi.

Ilidaiwa kwamba straika huyo wa zamani wa Manchester United ametofautiana na nyota wengi wa klabu hiyo katika chumba cha kuvalia, wakiwamo Marcelo na Fabio Coentrao.

Hata hivyo, imedaiwa pia kwamba Ronaldo anaona kwamba anahitaji mwanzo mpya kufikia malengo yake na kwamba alifadhaishwa na tukio la kutoswa na UEFA kwa kumtaja kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta, kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa UEFA.
Post a Comment