DK. SHEIN AONGOZA HARAMBEE YA UCHANGIAJI WA WALEMAVU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk ali Mohamed Shein akitoa hotuba katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika leo katika hoteli ya Zanzibar Beach Ressort.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akitoa hotuba na maelezo kuhusu mfuko wa watu wenye ulemavu,katika hafla ya kuchangia mfuko huo iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akimkabidhi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zahra Ali Hamad picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Aman Karume iliochorwa kwa Mkono na ambayo imeuzwa shiling 1,200,000 katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Theopista Muheta aliempelekea Chek ya Shiling10,000,000.katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakipunga mikono kama ishara ya kupiga makofi kuwapongeza Watu wenye Ulemavu katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.
Kikundi cha Ngoma kutoka Chama cha Viziwi (CHAVIZA)wakitumbuiza katika kwea kucheza ngoma ya Chanzo katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.
Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohamed Shein (wakatikati) akipunga mkono kama ishara ya kupiga mako0fi kwa lugha ya Walemavu Viziwi katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar Beach Ressort.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

Post a Comment

Previous Post Next Post