Mkuu
wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye akifungua mashindano ya
Redd's Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Ssebo ambaye ni mmoja kati
ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012
na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo lililofanyika katika
hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo
Kinondoni jijini Dar na wametoa zawadi kwa washindi watatu waliopatikana
kwa kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima ndani ya Saloon yao.
Shindano rasmi la kumsaka Redd's Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika
Ijumaa tarehe Septemba 14, 2012 katika Ukumbi wa Cassa Complex uliopo
Mikocheni, Dar
Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.
Mshiriki namba 2, Ester Musa alionyesha kipaji cha kuimba.
Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha jinsi ya kubuni vazi.
Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi
Post a Comment