KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI ZANTEL YAINGIA MKATABA WA KUIDHAMINI TIMU YA MPIRA WA MIGUU AFRICAN LYON

Katika kuthibitisha kuwa kampuni ya simu yenye ubunifu zaidi nchini, Zantel, leo imetangaza kudhamini timu ya mpira wa miguu ya African Lyon katika mkataba ambao utapelekea mafanikio makubwa kwenye kuendeleza mchezo wa mpira hapa Tanzania, ndani na nje ya uwanja.
Ushirikiano huo wa kipekee utaifanya Zantel kuidhamini timu ya African Lyon na timu yake vijana, ambayo kila mwaka itawapeleka vijana wawili nchini Marekani kwa udhamini wa kimichezo na kimasomo.
Udhamini huu utaleta maendeleo ya kweli katika mchezo wa soka nchini kwa kuwapa nafasi vijana wenye vipaji nafasi ya kufanya majaribio katika viwanja na walimu bora zaidi duniani.
Kiupekee zaidi, timu ya African Lyon ina mahusiano ya moja kwa moja na timu mbalimbali za nje kama Seattle Sounders FC ya ligi kuu ya Marekani pamoja na chuo cha Louisiana ambacho kila mwaka kitatoa udhamini wa kimasomo na kimichezo kwa watanzania wawili lakini pia kina mpango wa kujenga chuo hapa nchini.
Fursa hii itatoa nafasi ya kipekee kwa vijana watakaopata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa viwango vya juu kabisa duniani, na mwaka huu mwakilishiishi wa Tanzania kwenda Marekani kwa udhamini kamili wa masomo na kimichezo ni bwana Jarufu Magese.
Katika mpango huo pia, makocha na wachezaji vijana pia watanufaika na kliniki za soka zitakazokuwa zikiendeshwa hapa nchini mara kwa mara na makocha kutoka timu za kimarekani kama Portland Trailblazers ya ligi ya kikapu ya Marekani pamoja na makocha kutoka timu ya Seattle Sounders.
Akizungumza wakati wa sherehe za utiaji saini, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Bwana Sajid Khan, alisema udhamini huo unaonyesha aina ya maendeleo ambayo Zantel inatarajia kwenye michezo hapa nchini.
“Kampuni yeyote inaweza kuweka nembo yake kwenye jezi ya timu na kusema ni wadhamini, lakini Zantel tunataka kwenda mbele zaidi, sisi tunataka ushirikiano, na hivyo viwili vina tofauti kubwa, ushirikiano huu utatupa nafasi ya kutangaza jina letu kwenye jezi, lakini kikubwa zaidi ni nafasi tutakayopata ya kuendeleza mchezo wa mpira hapa nchini’ alisiitiza bwana Khan.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa sherehe hizo, naibu waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo, Mheshimiwa Amos Makala amezipongeza pande zote mbili kwa makubaliano waliyoingia akisema ana hakika yatalisogeza gurudumu la michezo nchini.
‘Sisi kama serikali tunafurahia sana kuona ushirikiano wa namna hii ambao unalenga kuendeleza michezo na elimu kwa vijana hapa nchini. Binafsi nawapongeza Zantel kwa hatua yao hii kwa kutoa udhamini ndani na nje ya kiwanja huku dhamira kubwa ikiwa kuendeleza michezo ’ alisititiza mheshimiwa Makala.
Akizungumza kwa niaba ya African Lyon, Mkurugenzi wa Ufundi bwana Charles Oteino aliwasifu Zantel kwa udhamini wao huo akisema wao kama African Lyon watautumia vizuri ushirikiano huo kuhakikisha timu yao inakuwa mfano wa kuigwa hapa nchini.
‘Hakuna maneno yanayoweza kuelezea furaha yetu, na  hii imeionyesha Zantel kama kampuni inayooanagalia mbali zaidi ya kujitangaza kibiashara lakini kufanya uwekezaji wa dhati katika mendeleo ya soka la hapa nchini’ alisisitiza Otieono.
Chanzo:-  zantel-tanzania

Post a Comment

Previous Post Next Post