![]() |
Redondo |
Jitihada za chini zinaendelea kwa viongozi wa Simba SC, kuhakikisha wanamalizana na klabu ya Azam FC juu ya kiungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’, aweze kuichezea klabu hiyo katika Ligi Kuu.
Azam
inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina
mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani na ili kumuachia kiungo huyo
iliyemsajili kutoka Simba miaka mitatu iliyopoita, inataka dola za Kimarekani
50,000 ingawa Simba wamefika dola 20,000 ambazo pia wameomba kulipa kwa awamu.
Habari
zaidi zinasema kwamba, Simba nayo inataka dola 60,000, zaidi ya Sh. Milioni 80 kutoka kwa Yanga, ili
wawauzie beki Kevin Yondan. Simba imepinga Yondan kusajiliwa Yanga kwa maelezo
kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.
Vilevile
Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu
Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka
huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo
alilipwa dola 30,000 na nyingine 20,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake
ya kujiunga na klabu hiyo.
Nayo
Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu
Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya
Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga
Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam
kwa msimu wa 2012/2013.
Pingamizi
lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni
wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano.
Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa
Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
Pingamizi
nyingine Zaidi bofya hapa
Post a Comment