MTU MMOJA AKATWA KICHWA ZANZIBAR.

Mtu mmoja akatwa kichwa Zanzibar na hapa ndipo ulipopatikana mwili wa mtu kisimani ukiwa hauna kichwa. kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Aziz Juma Mohammed amesema mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Seif Othman Mkumbo mwenye umri kati ya miaka 70 na 80 amekatwa kichwa na mwili wake kutupwa katika kisima cha Kwa Raju Kikwajuni au sijui niseme Maisara. Jeshi la Polisi limemkamata kijana aitwae Salum Khamis Said akiwasaidia polisi kwa upelelezi zaidi juu ya tukio hilo.

Taarifa zaidi zinasema kwamba Mzee Seif hajaonekana kwa siku tatu katika eneo lake la kazi wakati kumbe alikuwa tayari ameshakufa na awali wa kujulikana mkasa huo ni watumiaji wa kisima hicho walisikia harufu mbaya katika maji wanayotumia na ndio kijana Salum ambaye ni mlinzi wa hapo sehemu ya baa ya kwa Raju alipowaita wasafishaji wa kisima na ndipo walipochungulia na kuona mwili wa mtu na wakaitwa polisi kuja kushuhudia na kutoa maiti hiyo ambayo ilikuwa tayari imeshaharibika hadi sasa kichwa chake hakijapatikana lakini polisi wanamshikilia kijana ambaye alikuwa akiishi na Mzee huyo

Post a Comment

Previous Post Next Post