 |
| Mrisho Ngassa (kulia) wa Simba akijaribu kumtoka mchezaji wa African Lyon wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
 |
| Emmanuel Okwi akimgeuza mtu... chezea Okwi wewe!? |
 |
| Emmanuel
Okwi akipongezwa na Amir Maftah (aliye mgongoni) baada ya kufunga goli
dhidi ya African Lyon wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
 |
| Kikosi
cha Simba kilichoanza dhidi ya African Lyon katika mechi yao ya
ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam jana. |
 |
| Kikosi
cha African Lyon kilichocheza yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
 |
| Benchi la Lyon jana |
 |
| Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic (kushoto) akifuatilia wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana
(Septemba 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
imeingiza Sh. 67,793,000.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF,
Boniface Wambura, mashabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo
ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
Mgawo
mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna
wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh.
3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi
ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi
uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh.
4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
Nayo mechi ya
ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba
15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh.
50,435,000.
Post a Comment