![]() |
| Akuffo akishangilia bao lake |
![]() |
| Akuffo akishangilia huku akifuatwa na Juma Nyosso kupongezwa |
![]() |
| Nassor Masoud 'Chollo' anatia krosi |
![]() |
| Chollo anatia krosi |
![]() |
| Okwi anashangilia bao lake |
![]() |
| Ngassa anafunga akiunganisha krosi ya Chollo |
![]() |
| Wachezaji wa Simba wakimpongeza Ngassa (16)n kwa kufunga bao la pili. Kushoto kabisa ni mtoaji wa pasi Chollo akimuwahi kumpongeza |
![]() |
| Okwi anapasua |
![]() |
| Kikosi cha Lyon leo |
![]() |
| Kikosi cha Simba leo |
SIMBA SC
imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni
hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi
hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi
mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na
Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Mrisho Ngassa
dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, ambayo tayari
ilikuwa na mwelekeo wa kutinga nyavuni.
Lyon
walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na
Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha
pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala
mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffo aliifungia timu yake bao la kuhitimisha
ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la
hatari.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna
Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na
Emanuel Okwi.
African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi
Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa,
Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.
Katika mechi
nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul,
Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar
Khalfan, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu na Stefano
Mwasyika.
Kwenye Uwanja
wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa
1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni,
Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao/Jabir Aziz, John
Bocco, Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.
Kwenye Uwanja
wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41
liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.
Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na
Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.
Uwanja wa
CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT
Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting
mabao 2-1.
MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO
Simba 3 -0 African Lyon
Kagera Sugar
0 -1 Azam
FC
Prisons 0 -0 Yanga
Coastal
Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African
1 - 1 JKT
Oljoro
Polisi Moro 0 - 0
Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 2 - 1 Ruvu Shooting










Post a Comment