Ndg. Dimitries Mgalami akimsindikiza Mhe. Spika katika hotel itakayofikia wakati wote wa Mkutano huo wa CPA.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda amewasili Mjini Colombo nchini Sri Lanka
kuhudhuria Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya
Madola Dunian (CPA). Mkutano huo wa mwaka unafanyika Nchini humo
kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012, ambapo zaidi ya wabunge 1000
na Maspika wa Mabunge zaidi ya 80 kutoka nchi mbalimbali wananchama wa
jumuiya ya Madola watahudhuria mkutano huo wa mwaka.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia
ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito
Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad
Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9
zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo.

kamimu
Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano
wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami akiteta
jambo na Mhe. Spika mara baada ya kumpokea alipowasili Colombo Sri Lanka
kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa CPA unaofanyika Nchini humo kuanzaia
tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012.

Mjumbe
wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mhe. Okupa
Elijah kutoka Bunge la Uganda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege colombo Sri lanka kuhudhuria mkutano wa 58 wa CPA. aliyeko pembeni
ni Mbunge kutoka Uingereza.Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Post a Comment