Mkurugenzi
wa Idara ya Utafidi, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo,
akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jumatatu, kulia ni Katibu Mkuu wa
CAJAtz, Hassan Bumbuli na kushoto ni Mtoa Mada, Benedict Chale kutoka
TPDA.
************************
Na Mwandishi Wetu
Wasanii
nchini wametakuwa kuboresha namna ya utumiaji wa njia mbalimbali za
mawasiliano zinazopatikana hapa nchini na katika maeneo yao ili
kujitangaza na kutafuta masoko ya kazi zao.
Hayo
yamesemwa katika Jukwaa la Sanaa, na Mkurugenzi wa Kituo cha Wakala wa
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TPDA), Benedict Chale wakati
akiwasilisha mada ya umuhimu wa Mawasiliano katika Sekta ya Sanaa hapa
nchini.
“Tunatumia
vipi fursa kubwa ya mawasiliano iliyopo katika shughuli zetu za sanaa?
Hili ni swali la msingi, ukweli ni kwamba kumekuwa na tatizo la jinsi ya
kutumia fursa hizi za mawasiliano kiufanisi. Ni muhimu sana wasanii
wakaboresha namna ya kutumia haya mawasilinao katika kufanikisha kazi,
kujenga mtandao, kutafuta na kuimarisha masoko na mambo mengine ya
muhimu,” alisema Chale.
Alisema
licha kuwepo kwa unafuu mkubwa katika mawasiliano kuanzia katika simu
hadi intanet bado wasanii wanashindwa kutambua mbinu hasa za kutumia
nafasi hiyo kufanya mawasilino yatakayowaletea manufaa zaidi na kuwataka
kubadilika.
“Nawaomba
wasanii washiriki pia katika maonyesho ya kazi mbalimbali za wasanii
wengine na wajasiliamali, kufanya hivyo ni kuongeza wigo wa
mawasiliano, wengi wakiona ni maonyesho na picha basi mwigizaji haendi,
basi isiwe hivyo, tenga muda nenda kunafaida fulani utaipata tu,”
alisema.
Akihitimisha
mjadala wa Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa BASATA
Godfrey Lebejo, alitoa wito kwa wasanii kutumia pia fursa ya uwepo wa
mawasiliano rahisi kujitafutia maarifa na ujuzi kutoka katika mitandao
mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga urafiki na wasanii katika maeneo
mbalimbali Duniani.
Post a Comment