BAADA YA KOCHA DENMARK KUMWAGA UGALI, MTILIGA AMWAGA MBOGA



Football | World Cup 2014

Patrick Mtiliga

BEKI wa kimataifa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Patrick Mtiliga amesema kwamba aligoma kuingia akitokea benchi kwenye mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Italia, kwa sababu hakufurahia kuanzishiwa benchi kwenye mchezo huo.

Kocha Morten Olsen alisema juzi kwamba alishangazwa mno na beki huyo mwenye umri wa miaka 31 kukataa kupasha ili aingie kucheza akitokea benchi.

Amesema katika maisha yake yote ya kuwa kocha wa timu ya taifa, Mtiliga hatacheazea tena Denmark.

"Nilisikitishwa mno na nilifikiri ni kudharauliwa," alisema Mtiliga baada ya mazoezi leo. 

"Ningemudu hilo vizuri na kwa mawasiliano mazuri," alisema beki huyo anayechezea klabu bingwa Denmark, FC Nordsjaelland. Wenyeji Italia walishinda 3-1 Jumanne.

Post a Comment

Previous Post Next Post