Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa
akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya
Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea
kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya
Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
Habari ifuatayo imeandikwa na Ramadhan Ali na Mwanaisha Mohammed-Maelezo
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Bububu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama sheria za nchi zinavyowaelekeza.
Amesema mpaka hivi sasa watu 10 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliyotokana na vurugu za jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa Sheikh Farid unaendelea.
Ameongeza kuwa kutekwa kwa Sheikh Farid kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka kwake kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said ambae alikuwa dereva wake katika hatua za mwisho maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua umeme.
“Sheikh Farid alimuamuru Said amuache katika eneo hilo aende nyumbani kupeleka umeme na wakati huo akaendelea na mazungumzo na watu wengine walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya NOAH ambayo nambari zake hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.
Amesema fujo hizo zilisababisha hasara kubwa kwa Serikali, Chama tawala na wananchi ikiwemo kuchoma na kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani za CCM za Kisonge na Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari kuvunjwa vioo na kuvunja duka la pombe na kuiba mali iliyokuwemo ndani.
Hata hivyo amedai hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, na kutoa taarifa za watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya Coplo Said Abdulrahaman.
Mwisho IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
(picha via Happiness Katabazi blog)
Sheikh Ponda akiwa mahakamani Alhamisi, Otoba 18, 2012. (picha: K-VIS blog)
Sheikh Issa Ponda (katikati) akiwa na
wenzake 38 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
mapema leo walipofika kusomewa mastaka ya makosa yanayowakabili (picha:
Mtaa kwa Mtaa blog)
Habari ifuatayo imeandikwa na Happiness Katabazi, via blog, Dar es Salaam
HATIMAYE Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T), Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa wanausalama kwa kosa la uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Shilingi milioni 59.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilishwa mahakamani hapo hati ya kuzuia Ponda asipewe dhamana chini ya kifungu cha 84(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungi hicho kinampa mamlaka DPP kufunga dhamana kwa mshtakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika na mahakama inakuwa imefungwa mikono hivyo mahakama inakuwa haina mamlaka ya kuipinga hati hiyo ya DPP hadi pale siku DPP atakapojisikia kuiondoa mahakamani hati hiyo.
Washitakiwa hao 50 ambao wanawake ni 12 na wanaume ni 40 wakati mshitakiwa wa nne ni mwanamke aitwaye Zaida Yusuf mwenye umri wa miaka 100, na wanatetewa na wakili wa kujitegemea Nassor Mansoor ambao wakati wanaingizwa na kuondoka kwenye viwanja vya mahakama hiyo ndani ya magari ya polisi na jeshi la Magereza walikuwa wakisikika wakipaza sauti wakisema ‘Allah akbar, Allah akbar’.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wamevalia kombati huku wakiwa wamebeba silaha nzito na makachero wengine wakiwa wamevalia nguo za kiraia walianza kutanda ndani na nje ya viwanja hivyo tangu asubuhi na walifikisha mahakamani hapo washitakiwa hao kwa awamu mbili tofauti.
Awamu ya kwanza ilikuwa ni ya msafara wa magari matatu aina ya Defenda lenye namba za usajili PF 2118 na Z 442 BZ lilokuwa limebeba askari wa doria na Karandinga aina ya Layland lenye namba za usajili STH 2508 ambalo gari hilo lilikuwa limewabeba washitakiwa wake kwa waume 49 ambao walikuwa wamevalia baibu,na baadhi ya wanaume walikuwa wamevalia kanzu na vilemba kichwani maarufu kama ‘haghal’ wengine zikiwa zimechanika na wengine wakionekana kushindwa kutembea kwasababu ya majeraha waliyokuwa nayo miguuni na wengine walionekana kushindwa kukaa kwa muda mrefu kwenye viti vya mahakama hiyo na hivyo kukaa chini ya sakafu ambao uliwasili mahakamani hapo saa 5:16 asubuhi na kupelekwa moja kwa moja kuketi katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo.
Kisha msafara wa pili ambao ulikuwa na magari manne yenye namba za usajili PT 0886 gari lilobeba maji ya kuwasha ambalo ambapo katika msafara huu ndiyo uliwasili mahakamani hapo na mshitakiwa wa kwanza Ponda saa 6:23 mchana chini ya ulinzi mkali wa makachero zaidi 20 na kisha kumpitisha mlango wa nyuma ya mahakama hiyo na kumuingiza haraka ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama kwenda kuunganishwa na washitakiwa wenzie ambao waliketi ndani ya chumba hicho mapema tayari kwaajili kuanza kusomewa mashitaka yao.
Hakimu Mkazi Stewart Sanga alivyoingia ndani ukumbi huo wa mahakama na kuketi katika keti chake kabla ya mawakili kuanza kuzungumza chochote alianza kwa kusema kesi hiyo mpya namba 245/2012 kuwa yeye siye hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo,uongozi wa mahakama hiyo umempanga Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kusikiliza kesi hiyo na kwamba hakimu Nongwa yupo kwenye semina hivyo ana udhuru na alivyomaliza kusema maneno hayo alimtaka Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka na Zeberi Mkakatu kuanza kuwasomea mashitaka washitakiwa hao.
Wakili Kweka alianza kueleza kuwa Sheikh Ponda peke yake anakabiliwa na makosa matano isipokuwa washitakiwa wenzake 49 ambao wanakabiliwa na makosa manne ambayo makosa yote yanadhaminika kwa mujibu wa sheria.
Alidai shitaka la kwanza ni la kula njama kinyume na kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012,kwamba Oktoba 12 mwaka huu, huko eneo la Chang’ombe Markasi washitakiwa wote walikula kwa nia ya kutenda kosa hilo.
Wakili Kweka alidai shitaka la pili ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni la kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kiufungu cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kwamba Oktoba 12 mwaka huu, huko Chang’ombe Markasi , kwa jinai wasipokuwa na sababu za msingi washitakiwa hao waliingia kwenye kiwanja kinachomilikiwa kampuni ya AgriTanzania Ltd kwania ya kujimilikisha kiwanja hicho isivyo halali.
Kabla ya washitakiwa hakubali au kataa shitala hilo Ponda aliripoka na kusema yeye anakanusha shitaka hilo na kwamba washitakiwa wenzake nao wanalikanusha shitaka hilo,jambo ambalo lilikataliwa na Hakimu Sanga ambaye alimrisha kila mshitakiwa ajibu shitaka hilo kwa kinywa chake ambapo kila mshitakiwa kwa kinywa chake alikanusha shitaka hilo kinyume na alivyokuwa anataka Ponda iwe kwa yeye kukanusha shitaka hilo kwa niaba ya wenzake.
Wakili Kweka alilitaja shitaka la tatu kuwa ni kujimilikisha kiwanja kwa jinai kinyume na kifungu cha 86 na 35 cha sheria hiyo na kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu huko Chang’ambe Markasi pasipo na uhalali wowote washitakiwa wote katika hali iliyokuwa ikipelekea uvunjifu wa amani walijimilikisha kwa nguvu ardhi ya kampuni ya Agritanza Ltd.
Shitaka la nne, wakili Kweka alidai ni la wizi ambalo ni kinyume na kifungu cha 258 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, na kuwa kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu, washitakiwa hao waliiba vifaa na malighafi,matofali 1500,nondo,Tani 36 za Kokoto vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh 59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza Ltd.
Aidha shitaka la tano Kweka alidai ni la uchochezi ambalo linamkabili Sheikh Ponda peke yake ambalo ni kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha sheria hiyo kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu katika eneo hilo la Chang’ombe Markasi kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T) aliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao kutenda makosa hayo na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Mheshimiwa hakimu pamoja na kuwasomea mashitaka hayo ambayo yanadhamana kwa mujibu wa sheria, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Elizer Feleshi kwa mkono wake amenituma kuwasilisha kwaniaba yake mahakamani hapo hati ya kufunga dhamana kwa mshitakiwa wa kwanza (Ponda) peke yake chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2012’alidai wakili Kweka.
Kwa upande wake wakili wa shitakiwa hao Mansoor alidai anashangazwa na DPP-Dk.Feleshi kuwawasilisha hati hiyo ya kumfungia Ponda dhamana wakati dhamana ni haki ya Kikatiba na kwamba hati hiyo ya DPP imetaja sababu mbili ambazo ni mosi kwaajili ya usalama na sababu ya pili ni maslahi ya jamhuri.Nakuongeza kuwa sababu hizo hazijafafanuliwa kwa mabana na kudai kuwa washitakiwa wameishakaa kwa muda mrefu rumande na kwamba mshitakiwa wanne ni mwanamke mwenye umri wa 100 hivyo anaomba wapatiwe dhamana.
Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Kweka alidai anashangazwa na hoja za wakili washitakiwa za kuikosoa hati hiyo iliyowasilishwa na DPP kwasababu kifungu cha 184(4) cha Sheria Makosa ya Jinai, kinasomeka wazi kuwa hati hiyo ya DPP hata mahakama haiwezi kuipinga na kwamba inapowasilishwa mahakamani hati hiyo mahakama inakuwa imefungwa mikono na kwamba mwenye mamlaka ya kuiondoa makamani hapo ni DPP mwenyewe siku atapoona inafahaa kuiondoa na sivinginevyo.
Hata hivyo hakimu Sanga alisema hivi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili; “Kama nilivyokwisha sema tangu awali naingia kuanza kusikiliza kesi hii kuwa mimi siyo hakimu niliyepangwa kusikiliza kesi hii ,aliyepangwa kusikiliza kesi hii ni Hakimu Victoria Nongwa ambaye yupo kwenye semina kwahiyo endapo pande zote mbili katika kesi hii mnataka kuwasilisha hoja zenu msubirini Hakimu Nongwa akimaliza semina yake mje muwasilishe hoja hizo mbele yake”alisema Hakimu Sanga.
Hata hivyo wakili washitakiwa Mansoor alionekana kutoridhishwa na jibu hilo aliinuka na kumuomba hakimu Sanga aiarishe kesi hiyo hadi leo ili washitakiwa 49 waletwe leo kwaajili ya kupatiwa dhamana kwasababu makosa yao yanadhamana lakini hakimu Sanga alisema haitawezekana kwasababu Hakimu Nongwa bado yupo kwenye semina na leo hatakuwepo mahakamani hapo na hivyo akaamuru washitakiwa hao warejeshwe rumande hadi Novemba mosi,kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Baada ya kesi hiyo kumaliza wanausalama walikuwa wamejazana kwa mtindo tofauti ndani ya ukumbi huo wa mahakama waliwataka waandishi wa habari na watu wengine watoke nje na ndani wabaki washitakiwa peke yake na wanausalama na kisha wakatolea mlango wa nyuma washitakiwa hao na kisha kwenye kuwapakiza kwenye mabasi ya Jeshi la Magereza, Karandika na Defenda tayari kwaajili ya kuanza safari ya kupeleka gerezani ambapo magari ya askari wa usalama Barabarani walilazimika kuifunga barabara iliyopakana na mahakama hiyo kwa muda kwaajili ya kuruhusu msafara wa zaidi ya magari saba yaliyokuwa yamebeba washitakiwa hao,wanausalama kuelekea gerezani.
Baadhi ya watu waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo ,walizungumza na gazeti hili walisema wamefurahishwa na hatua ya serikali ya kuwafikisha washitakiwa hao mahakamani kwani Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa Sheria na Katiba ya nchi na siyo sheria za dini ya Kiisilamu.

Baadhi ya wakina Mama wanaounganishwa na
mashitaka hayo wakijisitiri ili wasipigwe picha. Hapa walikuwa kwenye
chumba cha Mahakama. (picha: Mtaa kwa Mtaa blog)
(picha: K-VIS blog)
(picha: K-VIS blog)
(picha: K-VIS blog)
Watuhumiwa katika karandinga wakirudishwa mahabusu (picha: Mtaa kwa Mtaa blog)
Post a Comment