|
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans
Mlelwa (kulia), akimkabidhi Mahmoud Zubeiry aka BIN ZUBEIRY wa
bongostaz.blogspot.com (kushoto) mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 2, baada ya
kushinda tuzo ya Mwandishi bora wa blogs wa mashindano ya Copa Coca Cola. Wengine
katikati ni Meneja wa Sprite, Warda Kimaro na Katibu wa TASWA, Amir Mhando.
|
KAMPUNI ya Coca Cola Kwanza, leo imewapa tuzo Waandishi
watano wa Habari nchini, baada ya kuibuka vinara katika tuzo za Waandishi Bora
wa mashindano ya soka ya vijana kwa umri chini ya miaka 17, Copa Coca Cola
yaliyofanyika Julai mwaka huu.
Upande wa Blogs, bongostaz.blogspot.com ya
BIN
ZUBEIRY imeibuka kinara na kuzawadiwa Sh, Milioni 2 sawa na washindi
wengine, upande wa Televisheni, Jimmy Tara wa ITV, Radio, Amry Masare wa Radio
One, Magazeti, Japhet Kazenga wa Daily News na Mpiga Picha, Mohamed Mambo wa
Habari Leo.
Tuzo hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa
Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa, makao makuu wa kampuni hiyo ya vinywaji baridi,
Mikocheni, Dar es Salaam.
Mchakato wa kutafuta washindi uliendeshwa na Chama cha Waandishi
wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho leo kiliwakilishwa
na Katibu wake, Amir Mhando.
|
Baadhi ya Waandishi waliohudhuria wakiwa kazini |
|
BIN ZUBEIRY anapokea mzigo |
|
BIN ZUBEIRY anapokea mzigo |
|
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi |
|
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi |
|
Jimmy Tara anapokea mzigo wake |
|
Amry Masare anapokea mzigo wake |
|
Kazenga ana[pokea mzigo wake |
|
Meneja
wa Sprite, Warda Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla
fupi ya utoaji wa tuzo hizo, Mikocheni, Dar es Salaam, kulia ni Katibu
wa TASWA, Amir Mhando na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa (kulia).
|
Post a Comment