BOB HAISA AKANUSHA KUWA YEYE SIYO CHIZI KAMA WATU WANAVYODAI



Hii picha imesambaa kwenye mtandao wa Facebook ikimwonesha Bob Haisa akiwa kama chizi na kuzua maswali mengi kama ni kweli ama ni harakati tu za kufanya sanaa.

Picha hiyo imewekwa na mtangazaji wa Kiss FM, D7.


Baada ya kuona kuwa kila mmoja anazungumza lake, mwandishi wa habari hii  amemtafuta Bob Haisa ambaye baada kucheka sana aliposikia jinsi watu wanavyoizungumzia picha hiyo, amesema hiyo picha ni ya video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Wa Kukaya’

“Safari hii sikupenda kuweka madancers kwenye video, nimeamua kuigiza mwenyewe kama Pedeshee, Choka Mbaya nk."

Amesema video hiyo bado ipo kwenye hatua za mwisho kumalizika ili itoke.

Post a Comment

Previous Post Next Post