CCM+CUF+UAMSHO=MAAFA

CCM: Ndiyo yenye dola, mamlaka na madaraka ya kudhibiti uvunjifu wa amani, Wanauamsho walichoma kanisa ZNZ tangu May 2012 serikali ilitakiwa ikifute hiki kikundi kwani hakina uhalali wa kisheria matokeo yake hamna juhudi za msingi za kukinyamazisha kwani malengo yake hayaendani na its practices in the real world.
CUF: Baadhi ya viongozi wamekuwa mstari wa mbele(ni haki yao) kudai ZNZ kuwa nchi kamili inayojitawala, hii ni sahihi kabisa ila the way the present ina fuel na ku back up harakati za wanauamsho zinazokuja kupelekea fujoMjumuiko wa haya yote matatu yanaleta MACHAFUKO
Kwa kweli kinachoendelea nchini kinasikitisha na kuleta hofu kubwa na sintofahamu.
Leo tunasikia kuwa Askari Police amechinjwa huko ZNZ, hapa ndio tulipofikia, haya ni matunda ya Uongozi wa nchi hii wa kulea upumbavu wa wachache wanaotumia kivuli cha Dini kufanya mambo yao. Hawa wanaojiita Uhamsho siku za karibuni wamekuja juu sana wakihitaji ZNZ iwe nchi kamili.Inachosikitisha harakati hizi zinachangiwa mkono na viongozi wa vyama vya Siasa mfano Mh Jussa Ismail (Mji Mkongwe-CUF) aliyeamua hapa juzi juzi kujiuzuru nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF ILI AWEZE KUWA NA MUDA WAKUFANYA HARAKATI ZA KUJIRUDISHIA NCHI YAO. Infact ipo wazi kuwa process mzima ya Muungano ilifanyika kwa zima moto na shinikizo hii inaeleweka lakini hata hivyo hawa wanasiasa wanapoongea waangalie kwani kuna wanachi wanaoshindwa kuchanganua na kuona mbele, wanayachukua maneno yanoyotoka vinywani mwa hawa wahamasishaji kama yalivyo na hivyo wanakuwa fuelled na kupandwa na jazba kwa maneno ya viongozi wao na hivyo kusababisha fujo na uvunjifu wa amani.
Historically ZNZ ni nchi ya visasi, kutokana na vikundi vinavyokuwa na itikadi tofautitofauti kulikuwa (na mpaka sasa mizizi ipo) Asili ya umetoka wapi mfano Washirazi, Waasia, Waajemi, Wangazija, Waarabu, Wamakonde, Wabara, Wapemba nk, pia hawa walikuwa wafuasi wa vyama tofautitofauti mfano Hizbu, Umma Party, ASP, ZNP n.k. Kutokana na hivi vikundi kulikuwa na uhasama mkubwa sana na sintofahamu na hii inadhihirishwa pale Rais wa kwanza wa ZNZ marehemu Abeid Amani Karume alipowanyonga baadhi ya waasisi wa Umma party, team yake katika Serikali ya mseto.
Tofauti hizi ziliweza kuwa under control kwa kuunda Muungano kwani baadhi ya waasisi wa hivi vyama waliounda serikali ya mseto walihamishiwa Tanganyika na kupewa madaraka tofautitofauti ili kuua umoja wao ambao ungeweza kumpindua Karume.
Ninachotaka kusema ni kuwa hawa wazanzibar visasi ni kawaida yao, Tanganyika iliingia Muungano kwa gharama kubwa sana, Nyerere alikubali ku shoulder hayo matatizo ya ZNZ, aliweza kuwavumilia sana, ilifikia mahala Karume alianza ‘kumpotezea’ Nyerere kwa kutokubaliana naye Kuingiza fedha za ZNZ kwenye hazina ya Taifa, pale alipopigwa mkwara asithubutu kugusa fedha yenye kichwa cha Malkia wa Uingereza kwani sio za Muungano kama anataka achukue za madafu, Karume huyu alisema Muungano ni kama Koti lilkikubana livue, haya yote Nyerere aliyavumilia.
Sasa basi tunapaswa kuendelea kuvumilia mzigo wa Muungano? Kama Nyerere alivyovumilia? Serikali iliyopo madarakani ya Muungano inafanya vya kutosha kujaribu kutafuta maridhiano? Hapana. Mungano umekuwa mzigo mkubwa sana, binafsi nisingependa uvunjike bali uendelee kwa model itakayopendekezwa na Nchi zote mbili, lakini hata hivyo bado ninawasiwasi kama kutakuwa na utulivu kwani itakuwa kama ya Libya sio wote watakaopata kipande cha keki na hivyo wachache wataamua kuleta mayhem, hapa solution ni kuwaachia nchi yao. Ninaamini kuna faida kubwa sana kuwa na Muungano ukitaka kutazama kwa jicho la pili, lakini imefikia wakati inabidi tufike mahala na kusema mwanamke huyu nimejaribu kila inavyowezekana, amenishinda kwani matatizo yanapotokea ZNZ inachafua taswira nzima ya Tanzania, inakuwa ni matatizo ya watanzania na wala sio ya wazanzibar, hawa jamaa hamna haja ya kungangania kuwa nao kwani wataambukiza wabara waweze kuleta harakati hizo hizo wanazozifanya, wanaweza pia kuitumia bara kama base ya harakati zao huko ZNZ hii itatuathiri sisi.
Hawa jamaa wameamua, kwa kile wanachjoita “ZANZIBAR KWANZA, MUUNGANO BAADAE” Waachiwe nchi yao, huu ni uamuzi mgumu sana sio rahisi kwni najaribu kufikiria matattizo yatakayojitokeza pale watakapoachiwa, kama nilivyosema hawa wana historia ya kutendana, historia hiyo haitakoma, tutashuhuia kama tunachoshuhudia LIBYA leo, walidai Demokrasia wakafanikiwa kumtopa waliyeona anawabania, matokeo yake vikundi vilivyoshiriki sio vyote vilivyopata keki na hivyo wameamua kuingia msituni tena, wana tafunana wao kwa wao, hamna amni tena Libya, hili litatokea ZNZ tutake tusitake, bado nasikitika tutakuwa na mzigo wa kupokea wakimbizi, umoja wa mataifa kupitia UNHCR wajiandae kufungua kambi za wakimbizi kwani hawa hawatakuwa watanzania tena kipindi hicho. Inasikitisha maamuzi ambayo hayatazingatia amani na umoja yataigharimu ZNZ na Tanganyika.
Mungu wape busara viongozi wetu na wanaharakati wafanye maamuzi sahihi yatakayo kumbatia amani na utulivu uliopo, Mungu ingiza hekima yako ndani ya miyoyo ya wanahatrakati ili wafanya harakati zao kwa kujali na kuzingatia Amani ya nchi hii, Mungu wajaalie Vinongozi wa Serikali ya Tanzania waweze kufanya due diligence jinsi ya kushughulikia tatizo hili haraka na kwa umakini sana ili lisilete maafa yasiyotarajiwa Amen.

Post a Comment

Previous Post Next Post