
DE GEA AIKATAA REAL MADRID AKISEMA ANAFURAHIA MAISHA MAN UNITED
MALOUDA KARIBU KABISA NA MLANGO WA KUTOKEA CHELSEA
Florent Malouda anatumai kumaliza maisha yake Chelsea, baada ya
klabu ya Santos kuanza harakati za kumsajili winga huyo wa Kifaransa
mwenye umri wa miaka 32.
Kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 21, amesema anafurahia maisha
Manchester United na hatarajii kurejea Hispania, licha ya taarifa kwamba
Real Madrid wanamtaka.
Chelsea, Manchester United na Liverpool zote zilimfuatilia beki
wa pembeni wa Genoa, Mario Sampirisi, mwenye umri wa miaka 19, timu yake
ikicheza na AC Milan Jumamosi.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson inataka kumsajili beki wa
kimataifa wa Uruguay anayechezea klabu ya Paris Saint-Germain ya
Ufaransa, Diego Lugano, mwenye umri wa miaka 31.
MARK HUGHES KATIKA WIKI NGUMU
Kocha wa Queens Park Rangers, Mark Hughes anakabiliwa na wiki
ngumu na anaweza kufukuzwa kazi iwapo hatashinda mechi yake ya wiki
ijayo dhidi ya Reading.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce amesema mshambuliaji Andy Carroll,
mwenye umri wa miaka 23, bado anahitaji ulinzi zaidi kutoka kwa marefa.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemtaka Roy Hodgson kutomchukua
Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 20, katika mchezo wa kirafiki wa
England dhidi ya Sweden mwezi ujao.
Credit:- Bin Zubeiry
Post a Comment