
DIDIER DROGBA KUREJEA ENGLAND KUKIPIGA LIVERPOOL
Liverpool inataka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Shanghai
Shenhua, Didier Drogba, mwenye umri wa miaka 34, mara Ligi Kuu ya China
itakapomalizika wiki ijayo.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kumsajili winga wa Newcastle
United, Hatem Ben Arfa, mwenye umri wa miaka 25,baada ya kukubali
kumpoteza Theo Walcott Januari.
Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 22, anatakiwa na AC Milan
na klabu hiyo ya Italia iko tayari kuuza nyota wake kadhaa ili kumsajili
mshambuliaji huyo wa Manchester City.
STEWART ROBSON ATOA USHAURI WA BURE ARSENAL UBUTU WA BEKI
Stewart Robson amesema kwamba matatizo ya safu ya ulinzi ya
Arsenal yanaweza kumalizwa kwa ushirikiano wa pamoja nabaina ya Kocha
Msaidizi na beki wa zamani wa kati wa Gunners, Steve Bould na Kocha
Mkuu, Wenger.
Manchester United imemtambulisha Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep
Guardiola kama mtu ambaye wanataka arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson
atakapoondoka Old Trafford.
Kocha wa St Johnstone, Steve Lomas, mwenye umri wa miaka 38,
amesema kwamba hawezi kuzipuuza tetesi za yeye kuhusishwa na kuhamia
Burnley.
MANCINI ATAKA KIKAO NA MWENYEKITI MAN CITY, OFISA MPYA MTENDAJI
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini anataka kuzungumza na
Mwenyekiti, Khaldoon Al Mubarak na Ofisa mpya Mtendaji Mkuu, Ferran
Soriano ili kujua kama watarusiah sapoti yao kamili kwake, katika
kutafuta namna ya kumrudhishia mamlaka ya kwenye chumba cha kubadilishia
nguo.
Post a Comment