HIVI NDIVYO 3 - 1 ZILIVYOPATIKANA KATI YA SIMBA NA AZAM - TAIFA/ PICHA

Mwadini Ali akiruka bila mafanikio kuokoa mpira uliopigwa na Felix Sunzu na kuipatia Simba bao la kusawazisha katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.  

Kocha wa Azam, Boris Bunjak na Msaidizi wake, Kali Ongala wakishuhudia kipigo
Azam wakipiga ndiki kabla ya mechi
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akisali kabla ya mechi
Picha na Bin Zubeiry( http://bongostaz.blogspot.com/)

Kaseja akishukuru baada ya sala
Salum Abubakr akipiga mpira
John Bocco akielea kushangilia baada ya kufunga
Bocco akichechemea baada ya kuumia
Salum Abubakar katikati ya wachezaji wa Simba, Jonas Mkude kulia na Okwi kushoto
Benchi la Azam
Shomary Kapombe akimdhibiti Samir Hajji Nuhu
Kaseja akiwapanga mabeki wake wakati wa kona
Kipre Tcheche akimtoka Paschal Ochieng
Samir Hajji Nuhu akitafuta mbinu za kumtoka Kapombe
Kapombe baada ya kumpokonya mpira Nuhu anaondoka nao
Okwi akitafuta mbinu za kumtoka Ibrahim Shikanda wa Azam
Juma Kaseja akisujudu baada ya Simba kusawazisha bao
Simba wakipongezana baada ya bao la pili
Mkude akimiliki mpira
Ochieng akizungumza na Kaseja
Ngassa anasafiri
Himi Mao Mkami akimtoka Mwinyi Kazimoto

 

SIMBA SC imezinduka kutoka kwenye wimbi la sare katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufanikiwa kuichapa Azam FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba izidi kujitanua kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22, baada ya kucheza mechi 10, wakati Azam FC inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi tisa.
Mabao ya Simba leo yalitiwa kimiani na Emanuel Arnold Okwi mawili na Felix Mumba Sunzu Jr. moja, wakati la Azam lilifungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
Hadi mapumziko, tayari Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-1, Azam wakitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja.
Dakika mbili baadaye, Sunzu aliisawazishia Simba, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto.     
Kipindi cha pili Simba walirudi na moto wao na iliwachukua dakika tano tu kuhitimisha karamu yao ya mabao, baada ya Okwi kuwainua tena vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Mrisho Ngassa ndiye alikuwa nyota wa mchezo wa leo, kutokana na kuisumbua mno Azam, iliyomuuza kwa mkopo Simba miezi miwili iliyopita.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba/Ramadhan Chombo, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu/Ramadhan Singano, Mrisho Ngassa/Christopher Edward na Emmanuel Okwi.
Azam FC; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad na Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz/Abdi Kassim, Himid Mao/Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’/Khamis Mcha, Kipre Herman na Salum Abubakar.
Katika mchezo uliotangulia, Azam B iliifunga Simba B 1-0, bao pekee la Kevin Friday dakika ya 56.
Kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee la beki Mbuyu Twite, hilo likiwa bao lake la tatu tangu ajiunge na timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Kwa ushindi huo, Yanga imetimiza pointi 17, baada ya kucheza mechi 10 na inaendelea kusimama katia nafasi ya tatu.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati ya African Lyon na Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, Mgambo JKT na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili kati ya JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ochieng amelala kuondosha mpira miguuni mwa Kipre Tcheche, huku Amri Kiemba akiwa tayari kumsaidia
Mkude anaondoka na  mpira mbele ya Abubakr wa Azam, huku Amir Maftah akiwa tayari kumpa msaada
Bocco anamtoka Ochieng
Simba wakishuangilia bao la Sunzu
Rafu iliyomtoa nje Bocco, aligongana na Kiemba
11 wa Simba walioipiga Azam leo
Humud akiwa hewani na Sunzu
Ngassa anawatoka wachezaji wa Azam
Ngassa anamuwajibisha Said Mourad
Okwi akijiandaa kufunga bao la tatu
Mwadini pamoja na kufunhgwa matatu, lakini aliokoa ya kutosha
Ulinzi ulikuwa mkali, lakini Okwi alipiga mbili
Kiungo wa zamani wa Azam na Simba, Shekhan Rashid akishuhudia mechi hiyo. Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Azam, Heri Mzozo

Post a Comment

Previous Post Next Post