 |
| Wa
pili kutoka kulia mdhamini mkuu wa Coastal Union, Nassor Bin Slum akiwa
kwenye Uwanja wa Mkwakwani leo wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara dhidi ya Simba, ambayo iliisha kwa sare ya bila
kufungana. |
 |
| Mwenyekiti wa Friends O Simba, Zacharia Hans Poppe aliyeinua mkono |
 |
| Kutoka kulia Hans Poppe, Evans Aveva na Pamba |
 |
| Hans Poppe |
 |
| Ben Mwalala kulia |
 |
| Kocha Mkuu wa Costal, Ahmad Morocco kulia akijadiliana na Kocha wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali |
 |
| Makchaa wa Vituko Show |
 |
| Mashabiki wa Simba |
 |
| Waandishi wa Habari |
 |
| Waandishi wa habari. Katikati ni Mhariri Mtendaji wa Mwanaspoti, Frank Sanga |
 |
| Nahodha wa Simba Juma Kaseja akiwaongoza wachezaji wake kuingia uwanjani |
 |
| Haruna Moshi 'Boban' akifurahi na Juma Jabu wakati timu zinaingia |
 |
| 11 wa Simba walioanza leo |
 |
| 11 wa Coastal walioanza leo |
 |
| Felix Sunzu anasafiri |
 |
| Sunzu anashughulika |
 |
| Kiungo chipukizi wa Simba, Haroun Chanongo akipasua msitu wa mabeki wa Coastal |
 |
| Nassor Masoud 'Chollo' katika msitu wa wachezaji wa Coastal akipasua |
 |
| Chollo huyo |
 |
| Chollo huyoo |
 |
| Jerry Santo wa Coastal akijaribu kumdhibiti Chollo |
 |
| Mwisho wa safari ya Chollo |
 |
| Sunzu akidhibitiwa |
 |
| Chollo katika mishe |
 |
| Haroun Chanongo anateleza |
 |
| Haroun huyo |
 |
| Haroun anamtoka Saidi Swedi Nahodha wa Coastal |
 |
| Haroun anamuacha Swedi |
 |
| Haroun anatia krosi |
 |
| Hatari kwenye lango la Simba |
 |
| Juma Kaseja anadaka |
 |
| Hatari kwenye lango la Simba |
 |
| Paschal Ochieng anaokoa |
 |
| Jerry Santo katika msitu wa wachezaji wa Simba |
 |
| Suleima Kassim 'Selembe' wa Coastal akipagombea mpira na Haruna Moshi 'Boban' wa Simba |
 |
| Kipa
wa Coastal, Jackson Chove akidaka mpira mbele ya Daniel Akuffo wa
Simba. Kulia ni Nahodha Saidi Swedi akiwa tayari kutoa msaada |
 |
| Chove akiwadaka huku akiugulia maumivu ya kuumizwa na Akuffo |
 |
| Chove amedaka, Sunzu chini |
 |
| Sunzu anamiliki mpira mbele ya Razack Khalfan |
 |
| Razack Khalfan anasafiri, Sunzu ameangukia goti |
 |
| Wachezaji wa Simba na Coastal wakigombea mpira |
 |
| Cheki kazi hiyo |
 |
| Mapumziko, kila kila ikisema na Mungu wake...kulia Coastal, kushoto Simba SC |
 |
| Kiungo wa zamani wa Coastal, Titus Bandawe kulia akizungumza na Saad kawemba wa TFF |
 |
| Razack Khalfan anatolewa nje, hakurudi.. |
 |
| Shughuli |
 |
| Atupele Green wa Coastal akichanja mbuga |
 |
| Atuepele anajaribu |
 |
| Amri Kiemba anamtoka Saidi Swedi kulia |
 |
| Sunzu leo alishughulika sana |
 |
| Kaseja anasema na mabeki wake |
 |
| Santo anatoa pasi |
 |
| Kiemba anapasua |
 |
| Hatari kwenye lango la Simba |
 |
| Amir Maftah anasafiri |
 |
| Saidi Swedi cbini, baad aya kukumbana na Maftah |
 |
| Sunzu akidhibitiwa |
 |
| Sunzu aliupitia mira mikononi mwa Chove |
 |
| Chove anampiga mkwara Sunzu baada ya kuupitia mpira mikononi mwake |
 |
| Shughuli |
 |
| Uhuru Suleiman kulia |
 |
| Uhuru kulia |
 |
| Kazi kazi |
 |
| Hatari kwenye lango la Simba |
 |
| Kaseja anawapanga mabeki wake |
 |
| Haruna Moshi 'Boban' anamiliki mpira |
 |
| Selembe chini |
 |
| M ilovan hana hamu na Coastal |
 |
| Wenye Simba yao 'wakisikia baridi' |
 |
| Hapa Kaseja aliokoa bao moja la wazi sana |
 |
| Boban na Swedi wakipongezana baada ya mechi |
AZAM FC imepiga hatua kubwa kuelekea
kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kufuatia ushindi wa goli 1-0
dhidi ya Polisi mkoani Morogoro huku Simba ikidondosha pointi mbili
katika sare ya 0-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mechi ambayo
wenyeji walimaliza wakiwa 10.
Goli pekee kutoka kwa straika raia
wa Ivory Coast, Kipre Tchetche liliifanya Azam ifikishe pointi 16, moja
nyuma ya mabingwa Simba wenye pointi 17 huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa
wamecheza mechi moja zaidi ya Azam.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Coastal Union walilazimika kucheza dakika 25 za mwisho wakiwa 10 baada
ya straika wao nyota Nsa Job kutolewa kwa kadi ya pili ya njano katika
dakika ya 65.
Katika mechi nyingine za leo, kwenye
Uwanja wa Manungu, wenyeji Mtibwa Sugar walichapwa 2-1 na timu ya Mgambo
JKT ya Tanga, ikiwa ni ushindi wake wa pili mfululizo baada ya kuanza
na vipigo vinne mfululizo tangu ilipopanda daraja msimu huu.
Ruvu Shooting ilishinda 1-0 dhidi ya
African Lyon kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi na Prisons ililala
nyumbani 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Vikosi katika mechi ya Tanga vilikuwa:
Coastal:
Jackson
Chove, Said Swedi, Juma Jabu, Mbwana Hamisi, Jamal Machelanga/Ismail
Khamis, Jerry Santo, Mohamed Athumani/Daniel Lyanga, Selemani K
Selemani, Atupele Green, Nsa Job na Razack Khalfan/Lameck Mbonde.
Simba:
Juma Kaseja, Nassor Said 'Cholo', Pascal Ochieng, Shomary Kapombe,
Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu, Daniel
Akuffor/Salim Kinje na Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman.
Picha na:- Bin Zubeiry
 |
| Milovan baada ya filimbi ya mwisho |
Post a Comment