Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe
Katika
hali ambayo haikutegemewa na wengi, katibu wa itikadi na uenezi wa
CHADEMA wilayani Makete Bw. Sinene amekifagilia chama cha mapinduzi kwa
kusema kuwa kimejitahidi katika mambo yake ikiwemo kuwa na wanachama
wengi wilayani hapo kwa zaidi ya asilimia 90
Sinene
ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha zake alipoalikwa kuhudhuria
mkutano wa uchaguzi wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa shule ya
sekondari Iwawa wilayani hapo
Katibu
huyo alisema “nikilinganisha huko nyuma na hii leo kwa kweli chama
chenu kimejitahidi kwa zaidi ya asilimia 90, mna wanachama wengi na
mnaendelea kufanya mengi”
Awali
wakati akianza kutoa salamu zake alisema unapokwenda sehemu inabidi
utumie taratibu za eneo hilo, hivyo kulazimika kusema ‘CCM hoyeeeeeee’
hali iliyowafurahisha wajumbe wa mkutano huo wakiwemo viongozi wa CCM
Baada
ya kumaliza salamu zake hizo kulipelekea utani wa hapa na pale ikiwemo
kumvalisha kofia ya CCM ingawa alikataa kuivaa huku wengine wakitaka
kumpa shati la kijani, na sauti za kumkaribisha CCM zikisikika
Akizungumza
mara baada ya kiongozi huyo wa CHADEMA kumaliza kutoa salamu zake,
katibu wa CCm wilaya ya Makete Miraji Mtaturu alisema ni kweli chama
chake ni kikubwa na wapinzani watazidi kupata tabu kama alivyokiri
mwenyewe
“Ndugu
wajumbe kauli ya katibu mwenezi wa CHADEMA mmeisikia wenyewe, kwa
kawaida katibu mwenezi ni msemaji wa chama, hivyo kauli yake ni kauli ya
chama, nachopenda kumwambia hakuna haja ya kupoteza muda, njoo CCM
ndugu yangu” alidai Mtaturu
Kauli
hiyo ya katibu mwenezi wa CHADEMA ilizua gumzo miongoni mwa wanachama
wake waliokuwa nje ya ukumbi huo huku wakisikika wakisema amejimaliza
kisiasa na kuona hana haja ya kuendelea kuwepo ndani ya Chadema na
badala yake ahamie CCM aliyoifagilia
Kauli
hiyo pia ilitumiwa na wagombea wa CCM katika uchaguzi huo hasa wale
waliokuwa wakitetea nafasi zao akiwemo Mzee Mwamwala kwa kusema kuwa
“katika uongozi wangu nimefanya mengi mazuri hadi mmesikia mwenyewe
CHADEMA wanaikubali CCM na wasingeikubali bila uongozi wangu mahiri,
hivyo naomba kura zenu”
Pamoja
na kutumia fursa hiyo Mzee Mwamwala alishindwa kutetea kiti chake na
nafasi yake ilichukuliwa na Francis Chaula aliyepata kura 791 dhidi ya
Mwamwala aliyepata kura 155
Francis Godwin Blog

Post a Comment