KATIBU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA ASHAMBULIWA KWA BOMU.

Picha mbali mbali za tukio la kupigwa kwa bomu nyumbani kwa katibu wa bakwata mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo (Pichani akiwa Hospitalini) na baadhi ya vongozi wa ulinzi na usalama mkoa wa Arusha wakionngozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa kwenye matukio mbali mbali nyumbani na hospitalini jijini Arusha leo baada ya tukio la kupigwa kwa bomu kwa katibu huyo nyumbani kwake eneo la mtaa wa kanisani kata ya Sokon 1 jijini Arusha.(picha na zote na Mahmoud Ahmad).
Mahmoud Ahmad Arusha
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Zuberi Mwombeji  ameelezea tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha na kusema kuwa MNAMO TAREHE 25 mwezi huu  MUDA WA SAA 6:30 USIKU KATIKA MTAA WA KANISANI KATA YA SOKONI ONE ILIYOPO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA ABDULKARIMU  IDD JONJO (52) KATIBU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA NA NI MKAZI WA SOKONI ONE ALIJERUHIWA KWA MLIPUKO KATIKA VIDOLE VYAKE VITATU VYA MKONO WA KULIA PAMOJA NA KIDEVUNI
TUKIO HILO LILITOKEA CHUMBANI KWAKE KATIKA NYUMBA ALIYOPANGA AMBAYO INAMILIKIWA NA JAPHET S URIO. TAARIFA ZA AWALI ZINAELEZA KWAMBA, NDUGU ABDULKARIMU  IDD AKIWA USINGIZINI GHAFLA ALISHTUSHWA NA SAUTI YA KISHINDO KILICHOTOKEA DIRISHANI NA MARA BAADA YA KUAMKA ALIONA KITU KIKINING’INIA DIRISHANI NA ALIPOKIGUSA GHAFLA ULITOKEA MLIPUKO AMBAO ULIMJERUHI KATIKA MAENEO YA MWILI WAKE YALIYOTAJWA HAPO JUU.
KUFUATIA TUKIO HILO, ALIOMBA MSAADA KWA MAJIRANI AMBAO WALIMPELEKA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA MATIBABU AMBAPO MPAKA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO NA ANAENDELEA VIZURI.
 Kaimu kamanda alisema kuwa MARA BAADA YA JESHI LA POLISI KUPATA TAARIFA HIYO BAADHI YA ASKARI WALIKWENDA KATIKA ENEO LA TUKIO NA KATIKA UCHUNGUZI WA AWALI WALIBAINI KWAMBA MLIPUKO HUO ULIANZIA NDANI YA CHUMBANI HICHO NA KUTOKEA NJE USAWA WA SAKAFU NA UKUTA, PIA KUMETOKEA UHARIBIFU WA VIOO VYA DIRISHA MOJA NA VIPANDE VYAKE KUANGUKIA NJE NA PIA MADUMU MAWILI YA LITA 10 YALIYOKUWA NA MAJI YALIPASUKA KWENYE VITAKO VYAKE NA MAJI HAYO KUTAPAKAA KATIKA CHUMBA HICHO.
 Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa jeshi hilo alisema kuwa MPAKA HIVI SASA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO NA JESHI LA POLISI MKOANI HUMO LINAENDELEA NA UPELELEZI WA KINA ILI KUWEZA KUBAINI CHANZO, SABABU ZA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NA HATIMAYE KUWAKAMATA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.

Post a Comment

Previous Post Next Post