LIL WAYNE AZUNGUMZIA SWALA LAKE LA KUZIMA MARA MBILI MFULUIZO


Boss wa Young Money Lil Wayne amezungumza kupitia account yake ya twitter yenye wafuasi million 8.8 na kuwaambia kuwa yuko katika hali nzuri baada ya kulazwa hospitalini mara mbili ndani ya masaaa 24 tangu alhamisi (October 25).

Mshindi huyo wa tuzo za Grammy ameandika kwa ufupi na moja kwa moja kwenye point iliyokuwa inasubiriwa na fans wake kuhusu afya yake, japokuwa hakusema kilichomsibu hasa.

Alitweet “Thanx for all the prayers! I am good…” ilisomeka hivi tweet ya october 27 ya mkali huyo wa michano.

Hivi karibuni Lil Wayne alilazwa hospitalini mara mbili baada ya kupatwa na kile kinachosemekana kuwa ni “seizure” na mara ya mwisho alizima akiwa katika private jet na kulazimika kuahirisha safari ambapo ndege hiyo ilitua na Weezy kukimbizwa hospitalini kwa matibabu, na wengi kuunganisha ugonjwa huu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Lakini management ya Weezy ilitoa taarifa ambazo hazikujibu hasa rumors hizo zilizokuwa zinatapakaa kwenye mitandao mbalimbali, na ikasema alikuwa amepungukiwa maji na pia maumivu ya kichwa cha upande mmoja lakini haikutoa sababu hasa ya hali hii.

Post a Comment

Previous Post Next Post