Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal
akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma
Kikwete katika Hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ya kuchangisha
fedha kwa Wanawake Wajasiriamali ikiwa ni Kipindi cha Mwezi wa Wanawake
Wajasiriamali nchini wenye Kauli mbiu “Msichana Amka Ujasiriamali ni
Ajira” ambapo amewataka Wakinamama waliokwisha fanikiwa kuwaongoza
Wasichana na wajasiriamali wanaochipukia njia sahihi za kibiashara
zitakazowawezesha kufikia mafanikio katika biashara na kutumia ubunifu
wao kama rasilimali.
Pia amewataka Wanawake kuonyesha Upendo na kushirikiana kwani Wanawake ndio chanzo cha Maendeleo katika Taifa lolote.

Mjasiriamali
na Mkufunzi Bi.Namsifu Nyagabona akishirikishana uzoefu wa Biashara na
wanawake wajasiriamali katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali
iliyohudhuriwa na Wabunge Wanawake pamoja na Wake za Viongozi
uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.

Mjasiriamali
Rhoda Mwamunyange akitoa hamasa kwa wanawake katika Usiku wa Mwanamke
Mjasiriamali ulioandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwawezesha Wanawake Wajasiriamali ulioandaliwa na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) pamoja Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Mtaalam
wa Saikolojia na Ushauri Aunty Sadaka Ghandi akizungumza katika hafla
ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ambapo amewasisitiza Wanawake pamoja
na Masuala yote ya Msingi pia waangalie uwiyano baina ya Familia na
Biashara ambayo inaleta kipato katika Familia ili kuepukana na madhara
ambayo yanaweza kuwapata wanafamilia kutokana na kujali sana kipato na
kusahau Ulezi wa Familia.

Mwanzilishi
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Marvelous Flotea Ltd. Bi. Flotea
Massawe wa Kampuni inayojihusisha Handcraft Textile, Gift Accesories,
Home Textlite na Food Processing akizungumzia jinsi alivyoanza kwa
kufanya biashara ya kutandika Batiki chini maeneo ya Mnazi Mmoja na
kuibuliwa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) kupitia kitengo cha kuwawezesha
wajasiriamali ambapo mpaka sasa biashara zake ni nchini na nje ya nchi
zilizomwezesha kupata tuzo mbalimbali za Kimataifa katika biashara.
Aidha
amewataka Wanawake wanaochipukia katika ujasirimali kutokata tamaa na
kuwa na ubunifu na uthubutu katika biashara kwa sababu usaidizi upo
utakaowawezesha kutambulisha biashara zao ndani na nje ya nchi.

Meza
kuu ikisikiliza Shuhuda za Kinamama waliofanikiwa katika Biashara za
Ujasiriamali. Mgeni rasmi katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasirimali
Mama Asha Bilal (wa tatu kulia), Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda( wa
pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA Bi. Hulda Kibacha (kulia), Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira), Dk. Therezya Huvisa (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa
Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema (wa tatu kushoto).

Pichani
Juu na Chini ni Baadhi ya Wake za Viongozi, Wabunge Wanawake na
Wanawake Wajasiriamalia waliohudhuria hafla ya Usiku wa Mwanamke
Mjasiriamali iliyofanyika jijini Dar es Salaam Serena Hotel.





Meza
kuu ikipiga makofi kuwapongeza Wanawake wajasiriamali waliotoa mada na
waliofanikiwa na kuwezesha kwa kufanyika hafla hiyo ambayo ni mfano wa
kuigwa.



Post a Comment