Borussia Dortmund wakishangilia kuifunga Real Madrid |
MATUMAINI ya Manchester City kufuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamepungua baada ya Borussia Dortmund kuifunga mabao 2-1 Real Madrid nchini Ujerumani.
Matokeo hayob yanaipeleka Dortmund
kileleni mwa kundi mbele ya timu ya Jose Mourinho, wakati City wanashika
mkia wakiwa na pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu.
Robert Lewandowski alifunga bao dakika
ya 36, kabla ya Cristiano Ronaldo kusawazisha ndani ya dakika mbili,
lakini Marcel Schmelzer akawafungia wenyeji la ushindi dakika ya 64.
Marcel Schmelzer akiifungia bao la ushindi Dormund
Olympiacos walipata ushindi wa kwanza
wakitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Montpellier nchini Ufaransa na
kuongeza ugumu katika Kundi B, baada ya Arsenal kufungwa na Schalke.
Gaetan Charbonnier aliifungia
Montpellier dakika ya 49kabla ya Vassilas Torosidis kusawazisha dakika
ya 73 na Kostas Mitroglou aliyetokea benchi akafunga la ushindi dakika
za majeruhi.
Matokeo ya jana yanaipeleka Schalke
kileleni kwa pointi zake saba, wakiizidi moja The Gunners, na Olympiacos
inakwenda nafasi ya tatu na Montpellier inaburuza mkia.
Olympiakos wamejiweka katika nafasi nzuri
Malaga imeendeleza wimbi la ushindi
kileleni mwa Kundi C baada ya kuifunga AC Milan 1-0 na sasa inaongoza
kundi hilo kwa pointi tatu zaidi. Joaquin ndiye aliyefunga bao hilo
pekee dakika ya 64 kwa pasi ya Manuel Iturra.
Mechi nyingine ya Kundi C, Zenit St Petersburg waliifunga 1-0 Anderlecht nchini Urusi.
Alexander Kerzhakov alifunga dakika ya
72 kwa mkwaju wa penalti, baada ya Milan Jovanovic kuchezewa rafu kwenye
eneo la hatari na Alexander Anyukov.
Katika Kundi A, Porto imeendeleza rekodi yake nzuri ya asilimia 100 kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ureno.
Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
AC Milan walifungwa na Malaga ya Hispania
Katika Kundi A, Paris St Germain ilikwea nafasi ya pili kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dinamo Zagreb nchini Croatia, Zlatan Ibrahimovic akifunga la kwanza dakika ya 32 na Jeremy Menez akafunga la pili kabla ya mapumziko.
Post a Comment